Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Waziri Jafo Aingilia Kati Usafiri wa Wanafunzi wa Bweni

Imewekwa tar.: March 20th, 2020

Na Fred Kibano

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo (MB) amewaagiza wakuu wa wilaya kushirikiana na wakurugenzi wa halmashauri  kuhakikisha wanafunzi waliofunga shule kutokana na tishio la maambukizi ya homa ya virusi vya corona wanapata usafiri wa kurejea majumbani mwao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Jijini Dodoma leo, Mhe.Jafo amewaagiza Viongozi hao kuratibu zoezi zima la usafiri wa wanafunzi wa bweni kwa shule za msingi na sekondari ili waweze kurejea makwao kwa amani na utulivu badala ya kutangatanga maeneo ya vituo vya mabasi kama walivyoonekana kwenye baadhi ya maeneo ya miji kama stendi ya Msamvu Manispaa ya Morogoro wakihaha kutafuta usafiri wa kuwarejesha majumbani mwao.

“Niwatake Wakuu wa Wilaya wote, Wakurugenzi wa Halmashauri wote na Wakuu wa shule wote kwamba katika maeneo yenu hakikisheni wale vijana ambao bado hawajapata usafiri mpaka sasa mnaratibu vizuri usafiri wa kwenda majumbani mwao kwa usalama na amani”

Waziri Jafo amesema kwamba hatarajii kusikia au kuona wanafunzi hao waliofunga shule wanazurura stendi na kwenye mitaa kwa ajili ya adha ya usafiri wakati Mkuu wa Mkoa na timu nzima ya Viongozi wapo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wakiwemo wanafunzi.

“Sitarajii kabisa kusikia tena baada ya maelekezo haya kwamba vijana wanaendelea kutangatanga kwenye maeneo ya stendi au mitaani wakati Mkuu wa Mkoa yupo, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi yupo”

Aidha, amewataka Wakuu wa Shule kuwasiliana na vyombo vya Ulinzi na Usalama kupitia Wakuu wa Wilaya na   Wakurugenzi endapo linatokea tatizo lenye kuhitaji usaidizi wakati wa kufanya zoezi hilo kwenye maeneo yao.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo amewapongeza Wakuu wa shule za Kilakala kwa kuratibu vizuri usafiri wa mabasi ambapo waliondokea shuleni kwao kwa mabasi na kufikia hii leo wanafunzi wa kanda ya Kiteto na Simanjiro ndio waliobakia hali kadhalika Dodoma sekondari ambapo Mkuu wa shule alikodi mabasi kwa wanafunzi wote na wazazi kutuma nauli baada ya zoezi hilo kufanyika.  

Awali Waziri Jafo amesema tayari Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga aliiandikia barua Mikoa kuhusu maelekezo ya namna ya zoezi la kufunga shule na kuwarejesha wanafunzi majumbani mwao kwa utaratibu unaofaa.  

Ikumbukwe kuwa changamoto ya ugonjwa wa homa ya virusi vya corona (COOVID 19) umeikumba Tanzania na Dunia kwa ujumla ambapo Serikali inaendelea kukabiliana nao kupitia Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoo,  Vitengo vya Maafa na majanga nchini na Wadau mbalimbali wa ndani na nje na sasa shule zote za msingi, sekondari na vyuo vimefungwa kwa mwezi mmoja baada ya maelekezo ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

             

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.