Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Huduma za Afyamsingi zimeimarika nchini - Dkt. Biteko

Imewekwa tar.: March 25th, 2024


Na. Fred Kibano, Dodoma 

Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za afyamsingi nchini ili kuhakikisha hakuna mwananchi anayekosa matibabu hali tukielekea kwenye huduma ya afya kwa wote.

Dkt. Doto Biteko ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma leo tarehe 25 Machi, 2024 wakati akitoa hotuba kwa niaba ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita sekta hiyo muhimu ilitengewa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundombinu, kununua vifaa tiba, dawa, magari ya wagonjwa na kuajiri watumishi. 

“idadi ya vituo vya afya imeongezeka kutoka mwaka 2017 hadi 2024 jumla ya vituo vya afya 2799 vimejengwa, zahanati zimeongezeka hadi kufikia 1762, vituo vya afya 910 na hospitali 127, majengo ya kutolea huduma za dharura 83, na majengo ya wagonjwa mahututi 28, nyumba za watumishi 150, gharama za ujenzi na ukarabati zimefikia shilingi Bilioni 937.2 hii ni hatua muhimu ya kutaka kuimarisha huduma ya afya ya msingi” alisema Dkt. Doto Biteko.

Kuhusu vifaa tiba amesema shilingi Bilioni 364.7 zilitolewa kununua x-ray 289 na utra sound 190, wakati magari 328 ya shilingi Bilioni 52 kwa ajili ya usimamizi shirikishi na wagonjwa wa dharura yalinunuliwa pamoja na utoaji wa vibali vya kuajiri watumishi wa kada ya afya zaidi ya 18,000. 

Aidha, amewataka viongozi nchini kuwatia moyo na kutambua mchango wa madaktari bila kuchukua madhaifu ya wataalam wachache ambao sio waaminifu wanaotia doa sekta hiyo na badala yake wachache wanaokiuka maadili wachukuliwe hatua za kisheria.

Katika hatua nyingine Dkt. Biteko amewaagiza viongozi na watendaji kuhakikisha kuwa miundombinu ya afya inatunza, kutoa elimu ya afya na chanjo kwa jamii, kutafuta mbinu za kuajiri watumishi katika kada ya afya na kuweka mifumo thabiti mipango ya tathmini na ufuatiliaji ili kutambua maeneo ya kufanyia maboresho kwenye sekta ya afya.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (AFYA) Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema lengo la mkutano huo wa kimataifa ni kuweza kujadiliana, kubadilishana uzoefu, mbinu na namna ya kuboresha huduma za afyamsingi kwa lengo la kuelekea hudma ya afyamsingi kwa wote.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Moleli amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania alitoa jumla ya shilingi Trilioni 6.7 kwa ajili ya kuboresha Sekta ya Afya ikiwemo afya ya msingi na huduma ya mama pia amewaomba watendaji wa Sekta ya Afya kwenda kuboresha usimamizi kwenye maeneo yao ili kufanya vizuri zaidi. 

Naye Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania Bi. Elke Wisch ameipongeza Tanzania kupitia Wizara ya Afya na ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuendelea kuboresha huduma za afyamsingi ili kuhakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma, kupunguza vifo vya watoto pamoja na kuongeza na kuboresha huduma za afya kutoka kipindi cha mwaka 2010 hadi 2022.

  


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Msovela: Fanyeni Kazi Kama Timu Kuleta Maendeleo

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.