Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Halmashauri zaagizwa kujenga madarasa kukabili wingi wa wanafunzi

Imewekwa tar.: May 10th, 2021

Na Mathew Kwembe, Sengerema

Serikali imezitaka  Halmashauri zote nchini kuhakikisha  kuwa zinajenga madarasa ya kutosha ya shule za msingi na sekondari ili kukidhi ongezeko kubwa la watoto wanaojiunga na elimu hiyo kufuatia hamasa iliyotokana na sera ya elimu bila ada.

Akizungumza jana Wilayani Sengerema wakati akikagua shule tatu kati ya 15 mpya zinazojengwa na wananchi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.David Silinde amesema ni wajibu wa halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa zinashirikiana na wananchi kujenga shule hizo kwa kutenga fedha kutoka mapato yake ya ndani.

Amesema jukumu la Serikali kuu ni kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni kwa shule zinazochukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

Naibu Waziri amesema kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI ilikwishatoa maelekezo kwa halmashauri kuhakikisha kuwa zinatenga fedha kila mwaka katika mapato yao ya ndani kulingana na kiwango cha fedha kinachopatikana.

“Kwa mfano zile halmashauri zenye mapato ya chini ya shilingi bilioni moja na nusu zinapaswa kujenga madarasa 20 kwa mwaka, na halmashauri zinazoanzia mapato ya bilioni moja na nusu hadi bilioni tano zijenge madarasa 40 kwa mwaka, na zile halmashauri zenye mapato ya zaidi ya shilingi bilioni tano zijenge madasa 80 hadi 120 kwa mwaka,” ameeleza Mhe Silinde.

Naibu Waziri amefafanua kuwa hatua hii ya serikali inalenga kuondoa janga la wanafunzi kukaa chini, na kusomea chini ya miti kwa kuzingatia kuwa sasa hivi kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaofanyiwa udahili wa kujiunga na shule hizo.

“Tangu serikali ya hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli ilipoleta sera yake mpya ya elimu bila ada na kuongeza udahili mwingi kwa wanafunzi sasa hivi kwa mfano watoto waliopo darasa la sita leo nchi nzima takwimu tulizo nazo wako watoto 1,800, 000,” ameeleza na kuongeza:

“Sasa wastani wa watoto kufaulu nchi hii ni zaidi ya asilimia 80, kwa hiyo uki –calculate hiyo asilimia 80 unazungumzia karibu watoto watoto 1,400,000 hadi 1,500,000 watafaulu na itabidi warudi sekondari.”

Ameongeza kuwa uwezo wa sekondari zote nchini kubeba wanafunzi wa kidato cha kwanza ni kubeba wanafunzi 780,000 tu hivyo wanafunzi hawa watakapojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023, wanafunzi 700,000 watakosa madarasa.

“ Kwa hiyo ndiyo maana tumekuja na hayo maelekezo kuwa halmashauri ni lazima zijenge madarasa, na sisi serikali tumetafuta fedha kujenga shule 1000 ambazo zikikamilika tutakuwa na uwezo wa kuokoa wanafunzi 400,000,” amesema.

Amesema hata baada ya shule hizo 1000 kujengwa bado watoto 300,000 watakosa nafasi katika madarasa hayo, hivyo ni wajibu wa kila halmashauri kuhakikisha kuwa wanashirikiana na wananchi kujenga madarasa ya kutosha katika halmashauri zao.

Akizungumzia ujenzi wa shule 15 mpya za sekondari wilayani Sengerema, Mhe Silinde amempongeza Mbunge wa jimbo hilo Mhe.Hamis Tabasam kwa kuwahamasisha wananchi kutoka kata 15 za wilaya hiyo kujenga madarasa kwa ajili ya watoto wao.

Mhe.Silinde ameahidi kwamba mara tu ujenzi wa shule hizo 15 utakapokamilika atazipatia mabweni shule tano mpya zitakazochaguliwa na halmashauri ya wilaya  ya Sengerema kupokea wanafunzi wa kidato cha tano.

Katika ziara yake wilayani Sengerema, mbali na kutembelea miradi ya masoko,  na stendi,  Naibu Waziri ametembelea shule tatu na kuweka jiwe la msingi katika shule mpya za sekondari za kata za Nyambulukano, Ibondo na Ngoma.

 

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.