Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Halmashauri 3 Mkoa wa Dodoma zapatiwa milioni 343.9 kwa ajili ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi

Imewekwa tar.: June 15th, 2022

.


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji ya Maendeleo (UN Capital Development Fund-UNCDF) wanatarajia kutekeleza miradi yenye gharama ya shilingi milioni  343.9/=  kwa ajili kujenga uhimili wa athari za mabadiliko ya tabianchi (Local Climate Adaptive Living Facility - LoCAL).



Akifungua kikao kazi cha watekelezaji wa program hiyo leo  tarehe 15 June, 2022 Jijini Dodoma. Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. John Cheyo kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Tamisemi Bw.  Ramadhan  Kailima  amesema  Programu  hiyo ina lengo la kuwawezesha wananchi kujenga uhimili wa athari za mabadiliko ya tabianchi.



Bw. Cheyo   amesema program inatekelezwa katika Halmashauri 3 za Wilaya ya Chamwino, Mpwapwa na  Kondoa zikiwa ni sehemu ya Halmashauri za kuanzia utekelezaji wa Mradi (Pilot Districts) ambapo fedha hizo zitatumika kuwawezesha wananchi kukabiliana na athari za mabadilko ya tabianchi hususan  ujenzi wa miundombinu ya mifumo ya usambazaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya jamii majumbani na umwagiliaji.



Aidha ameziagiza Halmashauri zinazoanza kutekeleza programu hiyo   kuhakikisha wanatoa matokeo  bora ili kuinusuru jamii na kujenga imani kwa  wafadhili kwa kuwa kwa kufanya hivyo,kutatoa fursa kwa wadau wengine kujitokeza kwa lengo la utekelezaji wa mradi  huo nchi nzima



Wakati Huohuo mwakilishi kutoka  Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji na Maendeleo (UNCDF) Bi. Aine  Mushi amezitaka Halmashauri zitakazotekeleza mradi huo kuhakikisha zinafanyakazi kwa uadilifu, utendaji kazi uliotukuka na kujituma ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya Tabia nchi nchini.



Aidha amendelea kufafanua kuwa Programu hii ina lengo la kuwawezesha wananchi kujenga uhimili wa athari za mabadiliko ya tabianchi na kujiletea maendeleo yao kwa kuwezesha fedha kutoka katika vyanzo vya kitaifa na kimataifa kufika katika ngazi za chini kabisa kama inavyoelekezwa katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu – (SDGs) Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 na Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wa Mwaka 2021 – 2026.




Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.