Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Changamoto isiwe kisingizio katika utekelezaji wa majukumu yenu – Dkt. Msonde

Imewekwa tar.: December 29th, 2023

Na. Fred Kibano, Morogoro

Serikali imewataka Watendaji wa Sekta ya Elimu nchini kuacha visingizio wanapotekeleza majukumu yao bali watumie changamoto hizo kama fursa ya kuwaletea wananchi maendeleo na kuisaidia Serikali.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa mapema leo tarehe 29.12.2023 na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) Dkt. Charles Msonde wakati akifungua kikao kazi cha nusu mwaka cha watekelezaji wa Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (GPE LANES II) kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Manispaa ya Morogoro.

Dkt. Msonde amesema kwa mtendaji yeyote changamoto lazima zitokee katika utekelezaji wa majukumu yake na hapo ndipo anatakiwa kuzitatua kwa wakati kwani fedha za miradi alizopewa zinatakiwa kutumika kwa wakati ili kutatua changamoto za kielimu zinazoikabili jamii.

 “tuhakikishe kila mtu kwenye eneo lake anatimiza wajibu wake, simamieni vile mlivyopewa lakini ni lazima mshauri vizuri kitu kitokee” amesisitiza Dkt. Msonde.

Katika hatua nyingine Dkt. Msonde amesema Mradi wa GPE LANES II umefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na Serikali na hivyo watendaji wahakikishe fedha zote za miradi zimetumika kabla ya tarehe 15, Januari, 2023. 

“ni vizuri kuhakikisha kwamba fedha hizi zinapotolewa na Serikali ambazo ni masharti waliyokubaliana na Benki ya Dunia unatekeleza na kukamilisha miradi kwa mujibu wa masharti waliyoweka, fedha hizi zina deadline (ukomo wa matumizi) tarehe 15 Januari  na haitakubalika na haikubaliki fedha yoyote ikafika tarehe 15 Januari” amesisitiza Dkt. Msonde.

Kwa upande wake Michael Ligola Mwenyekiti wa kikao kazi hicho ambaye pia ni Afisa Elimu Mkoa wa Songwe amesema kikao kazi hicho kina lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa kazi zilizotekelezwa chini ya Programu ya GPE LANES II kwenye elimu ambapo baadhi ya Halmashauri na Taasisi zimefanya vizuri ijapokuwa taasisi chache zilipata changamoto ya utekelezaji wa miradi. 

Akitoa neno la shukrani Adam Shimatayo amemshukuru mgeni rasmi kwa kuwatia moyo kuendelea kufanya kazi pamoja na kutokuwa na hofu ya changamoto za elimu bali wazione kama fursa na kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuliendeleza Taifa.

Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (GPE LANES II) ulianza mwaka 2019/2020 na utakamilika Januari 15, 2024 ikiwa ni mwaka wa fedha 2023/2024 na Mradi mwingine mpya wa GPE Multiplier unatarajiwa kuanza.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MHE MCHENGERWA AWATAKA MA RC, DC KUONGOZA JOGGING KWENYE MAENEO YAO

    June 14, 2025
  • MANYARA NA MWANZA MABINGWA RIADHA MITA 800 

    June 14, 2025
  • HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU  KATIKA KUANDAA MIRADI YA MAENDELEO- ADOLF NDUNGURU 

    June 13, 2025
  • WAVU KWAENDELEA KUNOGA UMITASHUMTA

    June 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.