
KWAGILWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MTWARA, AWATAKA WATENDAJI KUHESHIMU MASAA YA KAZI
OWM–TAMISEMI, Mtwara
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Mhe. Reuben Kwagilwa, amefanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi ya Kata ya Shangani, iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani, na kubaini kuwa baadhi ya watendaji hawakuwa wamefika kazini wakati wa ukaguzi huo.
Akiwa katika ofisi hiyo, Mhe. Kwagilwa ametoa maelekezo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, akiwataka watendaji na wataalamu wote waliopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kuzingatia na kutekeleza ipasavyo kanuni za Utumishi wa Umma.
Amesisitiza kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya F.1 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009, watumishi wote wa umma wanapaswa kuwahi kazini kuanzia saa 01:30 asubuhi na kudumu kazini hadi saa 09:30 alasiri, ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha, Mhe. Kwagilwa amewataka viongozi wa ngazi zote kusimamia nidhamu kazini na kuhakikisha watumishi wanatekeleza majukumu yao kwa weledi, uwajibikaji na kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
Comments
Join the conversation
Please sign in to share your thoughts and interact with the community.

