logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

WAZIRI MCHENGERWA AWAFUNDA MA RC WAPYA

Na John Mapepele

Mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaapisha na kutoa maelekezo kwa viongozi kadhaa aliowateua ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kuwafunda.

Mhe. Mchengerwa amewataka kuzingatia maelekezo yote waliyopatiwa na Mhe. Rais huku akisisitiza kuwa wanatakiwa kuwatumikia wananchi kwa kuwa Serikali ni ya wananchi na wasisite kuwasiliana na Wizara wapatapo changamoto.

"Ndugu zangu nadhani mmeiona dhamira ya Mhe. Rais ya kuwataka kwenda kuwatumikia wananchi.Mimi siwezi kuongeza chochote nawaombeni mkayazingatie yale yote aliyowaelekeza" amesisitiza Mhe Mchengerwa

Katika hotuba yake baada ya kuwaapisha  Wakuu wa Mikoa hao wapya  Mhe. Rais ametoa maelekezo mahususi  manne ikiwa ni pamoja na kuwataka  kutunza amani na usalama wa  wananchi katika mikoa yao kwa kuzingatia  kuwa Tanzania inakwenda kwenye uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.  

Aidha amesisitiza kufanya usimamizi madhubuti wa fedha za Serikali  ili zitumike kwa kuzingatia thamani ya huduma au bidhaa zinazonunuliwa.

Pia amewaagiza kuhakikisha Wakuu wote wa Mikoa  nchini wanasimamià ukusanyaji wa mapato ya ndani bila kutumia nguvu.

Aidha ameelekeka kwenda kuwasikiliza wananchi na kusimama katikati yao huku akisisitiza  kujishusha kwa  wananchi.

"Kuna fedha nyingi lakini mara nyingi  uongozi wa wananchi unafikiria  kuwekeza katika vitu vingine badala ya kuwekeza katika mahitaji  ya wananchi.Mathalan katika baadhi  Halmashauri miundombinu mibovu lakini fedha inayopatikana inawekezwa katika biashara nyingine hiyo siyo sawa". Amefafanua Mhe Rais

Mkuu Mpya wa Mkoa wa Kigoma akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakuu wa mikoa wapya katika kikao na Waziri Mchengerwa aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Adolf Ndunguru na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia TAMISEMI amesema  wanakwenda kusimamia  maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Rais na kushirikiana na Wizara mama ya TAMISEMI ili kuwatumikia wananchi na kuboresha maisha yao.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora