logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

UJENZI WA UZIO KWENYE  SHULE, SERIKALI YAJA NA MKAKATI MAALUM*

OR- TAMISEMI
Serikali imesema tayari imeweka bajeti na michoro (Master Plan) kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule zote za Hsekondari za mikoa kama hatua ya kuimarisha ulinzi wa mali za shule na usalama wa wanafunzi.

Akijibu maswali kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais– TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa, Naibu Waziri Mhe. Dkt. Festo Dugange  ameliambia bunge leo Mei 09,2025 kuwa pamoja na hatua hiyo wakurugenzi wa halmashauri kupitia mapato ya ndani waendelee kutenga fedha za ujenzi wa uzio kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na mali za shule kwenye maeneo yao kadiri ya upatikanaji wa fedha.

Naibu Waziri Dugange ametoa maelekezo hayo wakati akijibu swali la Mheshimiwa Dkt. Angelina Mabula mbunge wa jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza aliyeuliza kuwa ni  lini Serikali itajenga uzio katika Shule za Msingi ambazo hazina uzio maeneo ya Mijini.
Katika majibu yake Naibu Waziri Dkt. Dugange amesema “Katika mwaka 2022/23 na 2023/24 serikali imetoa shilingi bilioni 5.57 kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule 185 za watoto wenye mahitaji maalumu, lakini pia  Vilevile, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekuwa zikitenga fedha kupitia mapato ya ndani kujenga uzio ili kuimarisha ulinzi katika maeneo yenye changamoto za kiusalama.”

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kura yako haki yako jitokeze kupiga kura