logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

TARURA KUANZA KUTANGAZA ZABUNI ZA MWAKA 2025/2026

Singida

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amewaagiza Mameneja wa Mikoa nchi nzima kuanza kutangaza  zabuni za mwaka wa fedha 2025/26.

Mhandisi Seff ameyasema hayo jana alipotembelea ofisi ya Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida pamoja na kuzungumza na Mameneja wa TARURA wa wilaya katika mkoa huo.

Amesema katika zabuni hizo zizingatie barabara zenye kipaumbele kwa wananchi na zile zenye changamoto za kupitika

Pia Mtendaji Mkuu huyo aliwasisitiza Mameneja kufanya matengenezo ya barabara  kwa wakati na  kuhakikisha miradi yote ya kwenye maeneo yao inaanza mapema.

Hata hivyo amewataka Mameneja wa wilaya kuandaa mipango ya kuboresha barabara kwa kuzingatia  vipaumbele.

Mhandisi Seff yupo Mkoani Singida ambapo jana tarehe 1 Mei, 2025 alishiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani na kupewa zawadi ya fedha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa kuwa Mfanyakazi hodari  wa TARURA kwa mwaka  2024/25.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora