logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

TANZANIA KOREA KUFANYA MRADI WA UPANUZI WA MFUMO WA GOTHOMIS

Na Angela Msimbira,  Seoul, Korea

Serikali ya Korea Kusini kupitia shirika la KOICA imeandaa Mkutano wa Kimataifa kubadilishana uzoefu kwenye kuboresha mifumo ya usimamizi wa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Mkutano huu umehusisha watalaam kutoka Tanzania na Korea ikiwa ni sehemu ya ushirikiano wa Mradi wa Kupanua matumizi ya Mfumo wa GOTHOMIS unaotelekelezwa Mkoani Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa Tanzania,  Mkurugenzi  Msaidizi - (Huduma za Lishe) Bw. Lutifrid Nnally, amesema ushiriki wa Tanzania unalenga kujifunza uzoefu wa Korea kwenye matumizi ya mifumo ya kidijitali katika huduma za afya.

Tanzania inatarajia kutumia uzoefu huo kufanya maboresho ya GOTHOMIS, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa kutumia teknolojia kama telemedicine, akili bandia (AI) na mifumo ya taarifa za kiafya.

Ushiriki huu ni hatua muhimu katika mageuzi ya sekta ya afya, hasa kwa maeneo ya vijijini, ili kuhakikisha huduma bora, za haraka na kwa gharama nafuu zinawafikia wananchi wote

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora