logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

Serikali yatoa Tsh. bilioni 30 kuwezesha ujenzi wa vituo vya afya kata za kimkakati

Serikali imetoa shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo mbalimbali ya kimkakati kwenye majimbo 120 yaliyoainishwa na waheshimiwa wabunge kupitia bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo (June 02, 2025) bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali ya waheshimiwa wabunge katika kipindi cha maswali na majibu kwa  niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Akijibu swali la nyongeza la Mhe. Dorothy Kilave mbunge wa jimbo la Temeke aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali katika kujenga kituo cha afya kata ya Sandali jimbo la Temeke Mhe. Dkt. Dugange amesema licha ya serikali kujenga vituo vya afya katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Temeke lakini itaendelea kutenga fedha ili kuhakikisha kata zote za kimkakati zinakuwa na vituo vya afya.

“Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya kote nchini na niwahakikishie waheshimiwa wabunge kuwa hii ni dhamira ya dhati ya serikali kuhakikisha inasogeza huduma za afya karibu na wananchi na itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga vituo vya afya katika kata zote za kimkakati”.  alisema Mhe. Dkt. Dugange.
Serikali yatoa Tsh. bilioni 30 kuwezesha ujenzi wa vituo vya afya kata za kimkakati.

Serikali imetoa shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo mbalimbali kwenye majimbo 120 yaliyoainishwa na waheshimiwa wabunge kupitia bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo (June 02, 2025) bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali ya waheshimiwa wabunge katika kipindi cha maswali na majibu kwa  niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Akijibu swali la nyongeza la Mhe. Dorothy Kilave mbunge wa jimbo la Temeke aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali katika kujenga kituo cha afya kata ya Sandali jimbo la Temeke Mhe. Dkt. Dugange amesema licha ya serikali kujenga vituo vya afya katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Temeke lakini itaendelea kutenga fedha ili kuhakikisha kata zote za kimkakati zinakuwa na vituo vya afya.

“Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya kote nchini na niwahakikishie waheshimiwa wabunge kuwa hii ni dhamira ya dhati ya serikali kuhakikisha inasogeza huduma za afya karibu na wananchi na itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga vituo vya afya katika kata zote za kimkakati”.  alisema Mhe. Dkt. Dugange.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora