
SERIKALI YASISTIZA UZINGATIAJI WA MIONGOZO KATIKA UJENZI WA VITUO VYA AFYA
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afya kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Dkt. Paul Chaote amewataka wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya kufuata Miongozo ya ujenzi inayotolewa ili kufanikisha utoaji wa huduma bora na salama kulingana na Sera ya Afya.
Dkt. Chaote ameyasema hayo kwa niaba ya Naibu katibu Mkuu OWM-TAMISEMI anayeshughulikia afya Prof. Tumaini Nagu mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa jengo la upasuaji katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi.
“Niwatake wasimamizi wa ujenzi kuhakikisha maelekezo yote yanayotolewa kwenye michoro inazingatiwa, majengo kama haya ya upasuaji utaratibu wake wa ujenzi ni muhimu sana kwa ajili ya kuzuia maambukizi” amesema Dkt. Chaote
Pia, Dkt. Chaote ameelekeza kuwepo kwa ushirikiano wa karibu kati ya Wataalamu wa Afya ambao ndio watumiaji wa miradi hiyo na Wahandisi wa Halmashauri wakati wa utekekelzeaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha mahitaji yote muhimu yanatekelezwa kwa ufasaha.
Aidha, Dkt. Chaote amewaelekeza Waganga Wafawidhi (MOs) wa vituo vya kutolea huduma za afya kuhakikisha kwamba wanawalipa watumishi stahiki zao kwa wakati ili kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika utoaji wa huduma
Comments
Please sign in to leave a comment.

