logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

Prof. Nagu awafunda madaktari, ampongeza Mhe. Rais kwa maboresho makubwa ya afya.

Na John Mapepele

Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia eneo la Afya, Prof. Tumaini Nagu amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kote nchini kuendelea kuzingatia  taaluma na kufanya kazi kwa bidii ikiwa  ni kusherekea mafanikio makubwa ambayo yamepatikana katika Sekta ya Afya Msingi yaliyofanywa na Serikali kwa kipindi cha miaka minne cha Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Prof. Nagu ameyasema  hayo leo wakati akitoa neno la utangulizi katika Mkutano Mkuu wa Waganga wa Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Jijini Dodoma ulioanza leo.

Prof. Nagu amempongeza Mhe Rais kwa maboresho makubwa aliyoyafanya katika kipindi kifupi cha uongozi wake na kuwataka madaktari hao kusimamia vizuri uwekezaji huo ili wananchi wa chini waweze kunufaika na huduma za afya zinazotolewa na Serikali kote nchini.

“Ndugu zangu sote tunatambua uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwa ajili ya watu wake, hususani katika Sekta ya Afya, kwa ngazi ya Afya ya Msingi ambako ndipo wananchi wengi walipo kwani zaidi ya 95% ya Wananchi ndipo wanapopata huduma za afya”  amefafanua, Prof. Nagu.

Aidha, amesema malengo ya mkutano huo ni kujadiliana mambo mbalimbali ikiwepo kuimarisha mfumo wa utoaji wa huduma za afya katika ngazi ya msingi, kuboresha namna za usimamizi wa rasilimali zilizopo vituoni pamoja na miundombinu, kuweka Mikakati ya pamoja kuboresha uratibu katika  ngazi ya Taifa, Mikoa na Halmashauri na kutekeleza mipango ya afya.

Naye, Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema Waganga wa Wakuu wa Mikoa na Halmashauri ni wadau muhimu sana katika kuandaa Sera mbalimbali za afya kwani wao ndio watekelezaji wakuu wa Sera hizo hivyo maoni yao ni muhimu sana.

Mkutano huo mwenye kauli mbinu ya “Wajibu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katika kuimarisha ubora wa huduma za afya kuelekea bima ya afya kwa wote” unatarajiwa kumfungulia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hapo kesho.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora