logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

Mhe. Rais Samia amtaka Prof. Nagu kuboresha  huduma ya afya ya msingi.

Na John Mapepele

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia eneo la Afya  katika Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Prof. Tumaini  Nagu kuhakikisha kwamba huduma ya afya ya msingi inaboreshwa kwa wananchi.

Mhe. Rais ametoa maelekezo hayo leo, Mei 24, 2025  Ikulu ya Dar es Salaam mara baada ya kumuapisha kushika washifa huu baada ya kumteua hivi karibuni.

Mhe. Rais amefafanua kwamba tayari Serikali imeshafanya maboresho makubwa  katika eneo hili kazi iliyobaki ni kuendelea kusimamia kikamilifu ili kuimarisha eneo hili.

" Toka mwaka 2020  Serikali imefanya mambo makubwa  katika eneo hili kuanzia kwenye ukarabati wa zahanati kongwe, vituo vya afya, ongezeko la  vifaa tiba na wataalam". Amesisitiza Mhe. Rais

Pia Mhe.Rais amemtaka Profesa Nagu kwa kushirikiana na viongozi atakaowakuta  kwenda kutafuta ufumbuzi wa matatizo  ya wananchi kwenye sekta hiyo muhimu kwa taifa letu.

Aidha, amemtaka katika utendaji wa kazi kupunguza urasimu  huku akizingatia miongozo, sheria na kanuni katika utendaji wa kazi.

Katika uapisho huo, Waziri wa  Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu, Adolf Ndunguru na Watendaji kadhaa wa Wizara pia wameshiriki.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora