
KWAGILWA AWAKUTA WATUMISHI HAWAJAFIKA KAZINI GAIR0, ATOA ONYO KALI
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Mhe. Reuben Kwagilwa, amefanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Gairo majira ya saa 2:10 asubuhi na kukuta baadhi ya Wakuu wa Idara na watumishi hawajafika kazini.
Baada ya kukuta hali hiyo Mhe. Kwagilwa ameendelea kusisitiza umuhimu wa watumishi wa Umma walio chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI kuripoti kazini saa 1:30 asubuhi kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni F.1 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009, ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa wakati na kwa ufanisi.
Akitoa maelekezo mbele ya viongozi wa Halmashauri hiyo amesema “Nimekuja kwa kushtukiza leo nina ziara katika Mkoa wetu wa Morogoro lakini nitakuwa Manispaa ya Morogoro. Nikaona nipite niangalie maelekezo tuliyoyatoa ambayo Waziri wetu wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Mhe. Profesa Shemdoe alinielekeza nitoe kwa nchi nzima ili watumishi wote wazingatie Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2009 kwamba ifikapo saa 01:30 watumishi wa Umma walioko katika Wizara yetu, OWM - TAMISEMI wanatakiwa wawe wamefika katika eneo la kazi.” Amesema Mhe. Kwagilwa.
Ziara hiyo ya Mhe. Kwagilwa imelenga kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu nidhamu ya muda kwa watumishi wa Umma, kuacha uzembe na kuwajibika kwa wakati, kwani kutotimiza hayo kutachelewesha huduma na kuathiri ustawi wa wananchi.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
Tangazo la kuitwa kazini ajira za TMCHIP 2025
Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Takwimu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI - 2024/25 -2028/29
Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji 2024
Kanuni za Uchaguzi wa mwaka 2024
Tangazo la Uchaguzi

