logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

Katimba:Serikali itawafikia vijana wapate elimu ya kudhibiti maambukizi ya VVU

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema Ofisi hiyo itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na wadau wa maendeleo kuhakikisha inawafikia vijana na kutoa Elimu ya tahadhari na Udhibiti wa maambukuzi ya Virusi vya UKIMWI katika jamii.

Mhe. Katimba ametoa kauli hiyo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa katika hafla ya uzinduzi wa awamu ya tatu ya mradi wa Timiza Malengo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya Tunasonga na Samia kutokomeza UKIMWI, katika uwanja wa Madini wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi.

Amesema mradi huo unalenga kumuelimisha kijana katika kujitambua na kuweza kujilinda na changamoto zinazochochea katika kujihusisha na tabia hatarishi zinazopelekea kupata maambukizi hasa ya virusi vya UKIMWI.

Aidha, Mhe. Katimba amewapongeza   watendaji wote kwenye mradi huo hasa  watumishi wa OR – TAMISEMI walioko kwenye Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoka Mikoa 10 na halamshauri 32 kusimamia mradi huo ili uendelea kuleta tija kwa maendeleo ya vijana wa Tanzania. 

Kwa upande wake, mgeni Rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, amesema kiwango cha ushamiri wa maambukizi ya UKIMWI kwa umri wa miaka 15-49 kimepungua kutoka asilimia 4.7 kwa mwaka 2017 hadi asilimia 4.4 kwa mwaka 2023.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Godwin Mollel amesema gharama za matibabu kwa waathirika wa UKIMWI ni kubwa hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari ili kuepuka maambukizi

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora