logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

FANYENI MSAWAZO SAHIHI WA WATUMISHI KATIKA SEKTA YA AFYA KATIKA HALMASHAURI ZENU – MHE. DKT. DUGANGE

OR - TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Mhe. Dkt. Festo Dugange amewalekeza  Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya msawazo wa watumishi wa sekta ya afya ili kukizi mahitaji ya wananchi wakati ambapo Serikali inaendelea kutoa vibali  vya ajira katika  sekta hiyo.

Dkt.  Dugange amesema hayo  tarehe 9 Juni, 2025  Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Selemani Jumanne Zedi, Mbunge wa Jimbo la Bukene aliyeuliza

Je, lini Serikali itamaliza tatizo la upungufu wa watumishi wa kada ya Afya - Bukene.

“Katika maeneo yote ya zahanati yenye mtumishi mmoja fanyeni msawazo sahihi wa ndani wa watumishi kutoka kwenye vituo vyenye watumishi wengi ili kuendelea kutoa huduma muhimu kwa  wananchi” Mhe. Dkt. Dugange

Serikali inaendelea kutoa vibali vya ajira kila mwaka, ambapo kuanzia mwaka wa fedha 2020/21 hadi 2024/25 jumla ya watumishi wa kada ya afya 34,720 wameajiriwa na kupangiwa vituo.

Amesema  katika kipindi cha mwaka  2020/21 hadi 2024/25 halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepangiwa jumla ya watumishi 111 ambao wamepangwa katika hospitali ya wilaya, vituo vya afya na zahanati. Kati ya hao, jimbo la Bukene limepelekewa jumla ya watumishi 59.

Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa sekta ya afya kwa awamu na kuwapanga katika maeneo yenye upungufu wa wataalamu hao ikiwemo halmashauri ya wilaya ya Nzega.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora