logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

CRICKET YAENDELEA KUSHIKA KASI UMITASHUMTA IRINGA

OR-TAMISEMI

Timu za mchezo wa Cricket  zimeendelea kuoneshana ubabe kwenye mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi, yanayoendelea kitaifa Mkoani Iringa.

Kwa upande wa Wavulana, timu ya Mkoa wa Morogoro  ilionesha ubabe baada ya kuifunga Dar es Salaam kwa mikimbio 132 kwa 63 kwenye mchezo wa awali uliochezwa katika viwanja vya shule ya Sekondari Lugalo juni 13, 2025.

Kwa upande wa Cricket Wasichana, timu ya mkoa wa Tanga iliibuka mshindi kwa mikimbio 44 dhidi ya Dodoma iliyopata mikimbio 42, katika mchezo mwingine uliofanyika kwenye uwanja huohuo wa Shule ya Sekondari Lugalo.

Mchezo mwingine wa kusisimua wa Cricket wavulana, ulizikutanisha Dodoma na Morogoro, ambapo matokeo yaliipelekea Dodoma kuibuka mshidi wa mikimbio 85 kwa 83.

Mchezo wa Cricket, unachezwa kwa mara ya kwanza katika UMITASHUMTA 2025, na mwaka huu unahusisha jumla ya mikoa minne ya Tanga,Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam.

Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA, yanaandaliwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora