• Contact us |
    • FAQ |
    • Complaints |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

The United Republic of Tanzania

President's Office Regional Administration and Local Government

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Mpango Miji Mkakati (TSCP)
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi
    • Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Shilingi Bilioni Tano Kuboresha Miji 45, wamachinga kunufaika – Mhe. Majaliwa

Posted on: November 30th, 2021

Na Fred Kibano, Mbeya

Serikali imesema shilingi Bilioni tano zilizozotengwa zitasidia kupanga mipango ya miji na majiji 45 ikiwemo maeneo ya biashara ambayo yanatumiwa na wamachinga hapa nchini.  

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa alipokuwa akiongea na wafanyabiashara wadogo (wamachinga) Jijini Mbeya kuwa changamoto zinazowakabili zinatambuliwa na Serikali na hatua stahiki zinachukuliwa.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa makundi yote wanapofanya kazi zao bila bugudha yoyote kama ahadi ya Serikali ya Awamu ya Sita ilivyoagiza.

Aidha, ameuagiza Wakala wa Barabara za Mijini na Vijini (TARURA) kuhakikisha wanatengeneza barabara zote zinazozunguka eneo la Uwanja wa ndege wa zamani na soko la Salanga ambalo linatumiwa na wamachinga Jijini Mbeya.

Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza wamachinga wote ambao walitelekeleza maeneo waliyopangiwa na Mamlaka ya Jiji la Mbeya hapo awali na kurejea tena baada ya kuanza kwa maboresho, wapatiwe nafasi za vibanda ili wafanyebiashara kwa kuwa Serikali inawajali wamachinga wote.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amesema Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI ilipokea maagizo ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kufanya upangaji wa wamachinga nchi nzima ili kuondoa kero zao ikiwemo maboresho ya maeneo ya kufanyia biashara.

“naomba niwahakikishie kuwa Serikali ina mpango kwa miji 45 kupatiwa fedha kutoka Benki ya Dunia, Jiji la Mbeya likiwa ni mojawapo kupatiwa fedha za kujenga barabara, stendi za kisasa na eneo hili la wafanyabiashara wadogo wadogo (Wamachinga) lipo kwenye mpango wa kupatiwa fedha za Benki ya Dunia itakayoanza mwakani kwa ajili ya kuboresha eneo hili” alisema Dkt. Dugange.  

Aidha, amesema  Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya na Mstahiki Meya wameitwa Ofisi ya Rais TAMISEMI Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kufanya tathmini ya mradi huu mapema iwezekanavyo ambayo itatatua kero ya wafanyabiashara wadogo wadogo.

Akitoa maelezo ya awali kabla ya hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Homera amesema  eneo la Uwanja wa ndege wa zamani na Soko la Salanga lilikuwa na changamoto nyingi na hivyo kupelekea wafanyabiashara ndogondogo kulikimbia lakini baada ya kuanza kuboreshwa wafanyabiashara hao wanaohitaji vibanda vya biashara eneo hilo wamerudi tena.

Mheshimiwa Homera amesema Mradi mpya wa kiwanda cha kusindika mboga mboga unaogharimu shilingi Bilioni moja na milioni mia sita unajengwa karibu na eneo hilo lakini utahitaji wafanyabiashara ndogo ngogo wapatao 200 na hivyo kutoa ajira kwao na wananchi wengine.

Mbunge  wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson ametoa ombi la kujengwa kwa barabara zenye kiwango cha lami kuzunguka eneo hilo na kuliinua juu kwa kuweka kifusi kwa kuwa mazingira ya eneo hilo ni chepe chepe kwani yanajaa maji kipindi cha masika.

Masanja Matondo Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wadogo (Machinga) mkoa wa Mbeya amesema wanaiomba Serikali kuwafanyia mpango wa kupata mikopo nafuu kutoka kwenye mabenki kwa ajili ya kujenga vibanda vyao vya biashara, kupata mikopo ya asilimia 10 kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa, mikopo maalum kwa ajili ya kuwakopesha wamachinga, pamoja na Serikali kuuagiza Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kujenga barabara zenye kiwango cha lami kuzunguka eneo hilo la Uwanja wa ndege wa zamani na soko la Salanga.



Announcements

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • View All

Latest News

  • SOMO LA TEHEMA LIMERAHISISHA UTOAJI WA ELIMU MASHULENI KUPITIA MEWAKA

    May 19, 2022
  • Bashungwa apongeza ongezeko la Mishahara kwa watumishi nchini

    May 18, 2022
  • WALIMU WAMEIOMBA SERIKALI KUENDELEA NA MAFUNZO YA MEWAKA

    May 17, 2022
  • BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA - GOLANI ILI IWEKEWE LAMI.

    May 14, 2022
  • View All

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
More Videos

Quick Links

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Related Links

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

World visitors tracker

world map hits counter

Location Map

Contact us

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    Postal Address: 1923 Dodoma - Tanzania

    Telephone: +255 262 321 234

    Mobile:

    Email: ps@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Started on: 27th. July 2015
click here

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.