• Contact us |
    • FAQ |
    • Complaints |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

The United Republic of Tanzania

President's Office Regional Administration and Local Government

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Mpango Miji Mkakati (TSCP)
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi
    • Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Halmashauri Mwanga Watakiwa Kukarabati jengo la Wagonjwa wa Nje

Posted on: January 17th, 2022

Na Fred Kibano, Mwanga Kilimanjaro

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange ameagiza kufanyika ukarabati wa jengo la wagonjwa wa nje katika Kituo cha afya Kisangara wilayani Mwanga kabla ya Aprili, 30 mwaka huu.

Kauli hiyo ya Dkt. Dugange ameitoa hivi leo baada ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo amesema miundombinu hiyo haivutii wagonjwa katika kutoa huduma bora lakini pia wanakusanya mapato yanayozidi shilingi laki nane kwa mwezi kutokana na malipo ya wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu katika kituo hicho

“sijaridhishwa na uchakavu mkubwa wa majengo haya ya OPD (wagonjwa wa nje) na sisi kama watawala tupo hapa na gharama za utengenezaji haizidi shilingi milioni moja na nusu kwa jengo la OPD peke yake, sasa sio busara na wala haipendezi kwa wananchi kupata huduma katika kituo hiki chakavu wakati mnakusanya shilingi laki nane kwa mwezi” alisema Dkt. Dugange.

Aidha, amewataka Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuchukua hatua kwa watumishi ambao wamekuwa wanalalamikiwa na wagonjwa wakati wakiwapatia huduma hali inayopelekea kupungua kwa hadhi ya utoaji wa huduma bora kwa jamii kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Dkt. Dugange amewaasa Viongozi wa kada ya afya na nje ya kada hiyo kusimamia nidhamu ya kazi kwani baadhi ya watumishi wachache wamekuwa na lugha isiyo na staha kwa wagonjwa na hivyo kuwakatisha tamaa kupata huduma kwenye vituo ambavyo watu hao hufanyia kazi.

“baadhi ya maeneo kumekuwa na malalamiko ya lugha zisizofaa kwa baadhi ya wahudumu wa afya wanaofanya kazi bila kufuata maadili, miongozo, taratibu na kanuni za utoaji wa huduma za afya, sasa tuwe na mfumo wa kufuatilia zahanati, kituo cha afya au hospitali inayolalamikiwa na wananchi”

Amesema ni muhimu kujua jambo linalolalamikiwa, sababu, watumishi wanaotajwa ili wawajibishe kwa mujibu wa sheria za kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bi. Mwajuma Nasombe amesema wameyapokea maelekezo ya Serikali na kwamba watayafanyia kazi kwa wakati kwa kuondoa kasoro zote zilizojitokeza.

Miradi mingine aliyotembelea Dkt. Dugange ni pamoja na barabara ya Cleopa David Msuya chini ya TARURA na shule ya sekondari Mandaka zote za wilayani Mwanga.


Announcements

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • View All

Latest News

  • SOMO LA TEHEMA LIMERAHISISHA UTOAJI WA ELIMU MASHULENI KUPITIA MEWAKA

    May 19, 2022
  • Bashungwa apongeza ongezeko la Mishahara kwa watumishi nchini

    May 18, 2022
  • WALIMU WAMEIOMBA SERIKALI KUENDELEA NA MAFUNZO YA MEWAKA

    May 17, 2022
  • BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA - GOLANI ILI IWEKEWE LAMI.

    May 14, 2022
  • View All

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
More Videos

Quick Links

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Related Links

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

World visitors tracker

world map hits counter

Location Map

Contact us

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    Postal Address: 1923 Dodoma - Tanzania

    Telephone: +255 262 321 234

    Mobile:

    Email: ps@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Started on: 27th. July 2015
click here

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.