Dkt.Chaula awaasa Wahandisi wa Maji Mikoa Kufanya kazi kwa Matokeo Chanya

Na.Fred Kibano

Chaula awataka wahandisi wa maji kuboresha utendaji wao

Naibu Katibu Mkuu (AFYA) ofisi ya Rais TAMISEMI, Zainabu Chaula amewaasa Wahandisi wa Maji wa Mikoa nchini kufanya kazi kwa weledi hali wakitambua majukumu yao bila kusukumwa kufanya kazi zao ili kuboresha sekta ya maji nchini.

Chaula ameyasema hayo wakati wa kikao kazi kilichowahusisha Wahandisi wa Maji wa Mikoa, Wahandisi kutoka Wizara ya Maji na Menejimenti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI. Amesema Sekta hiyo inahitaji kusimamiwa ipasavyo kama inavyotaka Ilani ya Chama Tawala la kuboresha Sekta ya maji vijijini na mijini kwani kwa kufanya hivyo hata afya za wananchi zitaboreshwa hususani kuondoa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.

"Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ni Mkataba kati ya CCM na Wananchi, lengo ni kuondoa changamoto zote za upatikananji wa maji, hii inapelekea kuhitaji watumishi wenye weledi" Chaula amewaagiza Viongozi hao kuendelea kusimamia watu walio chini yao kama Viongozi imara wasio sukumwa sukumwa kutekeleza majukumu yao kwani matokeo yanayoonekana ni kazi za watu wengine. "haya matokeo mnayoyaona ni jitihada za watu wachacheambao wapo committed" (wanajituma).

Aidha, amesema WIzara za Kisekta kama Wizara ya Maji inatunga Sera na baadhi ya Miongozo ambayo utekelezaji wake ni Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa maana ya Mikoa na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa.

kwa upande wake Mhandisi Enock Nyanda kutoka Idara ya Uratibu wa Kisekta OR TAMISEMI amesema Viongozi hao ambao ni wasimamizi wa Sekta ya Maji nchini wanajukumu kubwa kuona kwamba maeneo wanayoyasimamia yanatoa matokeo yanayotarajiwa, yakiwemo maji na usafi wa mazingira inayosimamiwa na OR TAMISEMI, miundombinu ya maji, uwasilishaji wa taarifa mbalimbali kwa kuzingatia viashiria vya upatikanaji wa maji.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.