JAFO AWAPONGEZA VIONGOZI WA MKOA WA SINGIDA UJENZI WA VITUO VYA AFYA

Na.Fred Kibano

serikali mkoani singida yaboresha vituo vya afya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Singida kwa usimamizi wa Miradi ya ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea mkoani humo hivi sasa.

Waziri Jafo ametoa pongezi hizo alipotembelea kukagua ujenzi wa kituo cha afya Kintinku kilichopo wilayani Manyoni mkoani Singida.

Waziri Jafo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho serikali imepeleka sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.

Amebainisha Mkoa wa Singida unaendelea ujenzi katika vituo saba ambapo kila eneo maendeleo ya ujenzi yanaenda vyema.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Manyoni mashariki Daniel Mtuka kwa juhudi zake za kuwahangaikiwa wananchi wa Jimbo hilo.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.