Waziri Jafo aigiza TARURA kujenga barabara ya chang’ombe - Mipango

Na Fred J. Kibano

Serikali yaagiza TARURA kujenga barabara ya lami

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo, ameagiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini TARURA) kuelekeza bajeti yao ya mwaka 2018/2019 kujenga barabara ya kilomita tatu kutoka Kata ya Chang’ombe hadi Chuo cha Mipango ili kutatua kero ya barabara kwa wakazi wa kata ya Chang’ombe mkoani Dodoma.

Mhe. Jafo alitoa maagizo hayo alipokua anazindua soko jipya la Chang’ombe lililojengwa na Serikali kwa kusaidiana na wafanyabiashara na Mbunge wa Dodoma mjini Anthon Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana.

Soko hilo ambalo lilianza kujengwa mwaka 2017 na kukamilika mwaka huu, hilo lina wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali takribani 342 ambapo wamesaidia kusogeza huduma kwa wananchi kupata bidhaa mbalimbali. Hata hivyo soko hilo bado linachangamoto mbalimbali kama ukosekanaji wa mifereji ya kutirisha maji, vumbi na ukosefu wa barabara za lami ili kurahisisha ushushaji wa mizigo sokoni kwa magari ya mizigo na abiria yanayoingia sokoni hapo.

Waziri Jafo alisema Serikali inawekeza miundombinu ya hali ya juu katika mkoa wa Dodoma mfano mtandao wa barabara za lami katika maeneo mbalimbali pamoja na taa za barabarani ikiwa ni pamoja na ujenzi wa dampo la kisasa. “Kwa kuwa serikari inahamia Dodoma hivyo basi miundombinu mbalimbali lazima iendelee kujengwa na kurekebishwa” Alisisitiza Mhe. Jafo

Waziri jafo aliwapongeza wananchi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa kukamilisha ujenzi wa soko la kisasa hali akiwapongeza na kusema “soko hili limejengwa kwa gharama nafuu sio kama masoko mengine yanayojengwa kwa gharama kubwa mno”

Ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na Mbunge wa Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde kwa jitihada zao za kuleta maendeleo mkoani hapo.

Alisisitiza wananchi wawe na vyanzo vya mapato lakini pia wafanye biashara mbalimbali ili kuinua kipato. Alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma wakamilishe masoko mbalimbali pamoja na kuanza kutumika kwa machinjio ya kuku yaliyopo soko la majengo, “kuku wachinjiwe palepale na sio sehemu nyingine” Pia aliwaasa wafanyabiashara kufanya biashara bila kuwekeana chuki ili kuleta maendeleo kwenye kata yao.

Amewaasa wananchi wawape Viongozi wa Serikali ushirikiano ili kutatua kero zinazowakabili na kuifanya Kata yao kuwa ya mfano katika Manispaa ya Dodoma.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.