Wakurugenzi Waagizwa kuandaa mazingira bora Ajira mpya za Serikali

Na. Nteghenjwa Hosseah

Waziri OR TAMISEMI aagiza Wakurugenzi kuandaa mazingira rafiki ya ajira za Serikali

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini kuandaa mazingira rafiki kwa watumishi wapya wanaopangiwa katika Halmashauri zao.

Simbachawene ameyasema hayo ikiwa ni wiki moja tangu kutangaza ajira mpya za Walimu wa Masomo ya Hisabati na Sayansi wapatao 3,081 wa ngazi ya Shahada na Stashahada ambao wamepangiwa kwenye Halmashauri mbalimbali Nchini.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msangambuya wakati wa Ziara yake ya Kikazi Wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe Mhe. Simbachawene amesema watumishi wengi wapya wanakatishwa tamaa na mazingira mabovu wanayoyakuta katika Halmashauri zao na hali hiyo huwatia hofu ya kuendelea kukaa katika maeneo hao.

Unakuta mtumishi anafika Halmashauri malipo yake hayajaandaliwa zaidi ya mwezi mzima, kisha anapangiwa kwenye Kata mbayo hata hajawahi kuifahamu hapo awali na hapewi hata maelekezo ya ziada ya namna ya kufika katika Kituo chake na unakuta wenyeji wake katika Kata na Shule hawana taarifa za ujio wa mtumishi huyo hivyo mtumishi anahangaika mpaka anakosa ari ya kufanya kazi katika kituo chake kipya alisema Simbachawene.

“Ninahitaji Kila Halmashauri kuandaa Malipo stahiki kwa ajili ya walimu wanaoendelea kuripoti hivi sasa katika maeneo mbalimbali, Usafiri wa kuwapeleka katika vituo vyao vya Kazi, mapokezi stahiki kwa uongozi wa Kata pamoja Shule sambamba na kuhakikisha anapata makazi bora ya kuishi katika eneo lake jipya la Kazi”.

Sitaelewa Halmashauri ambayo itashindwa kuzingatia maagizo haya kwa namna yeyote ile na nitaendelea kufuatilia mazingira ya mapokezi ya watumishi hawa, sitaki mtumishi yeyote ashindwe kufanya kazi yake kwa ufanisi kwa sababu ya mazingira magumu anayokutana nayo wakati wa kuripoti kazini, Aliongeza.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi. Eliachi Macha alisema Halmashauri imeandaa mazingira mazuri kwa ajili ya mapokezi ya walimu wapya na pia watahakikisha wanatekeleza maagizo yote ili watumishi wote waweze kufanya kazi za ujenzi wa Taifa na kuleta matokeo chanya.

Naye Diwani wa Kata ya Mtera Mhe. Amon Kodi ambaye alishiriki katika ziara hii alimpongeza Waziri Simbachawene kwa kazi kubwa anayoendelea kufanya katika Kata yao, Jimbo la Kibakwe na Taifa kwa Ujumla na kumshkuru kwa kufanikisha utekelezaji wa Miradi ya ujenzi wa bweni la Mtera Sekondari, ukarabati wa zahanati ya Kisima pamoja na ukarabati wa matundu ya vyoo vya Shule vya Msingi Msangambuya.

Mhe. Simbachawene yupo katika ziara ya Kikazi Wilayani Mpwapwa, Jimbo la Kibakwe na ametembelea Kijiji cha Msangambuya, Chamsisili pamoja na Chinoje.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.