Watumishi OR TAMISEMI washauriwa kufanya kazi kwa weledi

Na. Shani Amanzi, Enock Mhimbano na Sylvia Hyera

Watumishi OR TAMISEMI washauriwa kufanya kazi kwa weledi

Watumishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kufuata kanuni na sheria katika utendaji kazi ili kufanikisha utekelezaji wa ilani ya chama Tawala na kutimiza wajibu wa kuwatumikia wananchi .

Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Afya,Dkt Zainabu Chaula wakati wa uzinduzi wa JUMA LA OPRAS na uliofanyika leo katika viunga vya Wizara.

Alisema kuwa kila mtumishi anatakiwa kufanya kazi kwa kufuata Sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma katika kufanikisha malengo na mikakati iliyowekwa na Taasisi husika.

‘’ Kwa kupitia mfumo huu wa OPRAS ambao ni mfumo wa wazi katika kufanya tathmini ya utendaji kazi wa kila mtumishi naamini sasa kila mtu atatimiza majukumu yake ipasavyo “alisema

Aidha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Bw. Tixon Nzunda aliwataka watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali kushirikiana katika kutekeleza dhana ya mabadiliko katika utumishi wa umma.

Alisisitiza kuwa mfumo uliokuwa ukitumika uliwafanya watumishi wengi kutokuwa na malengo katika utendaji kazi hivyo kukosa dira ya namna ya kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali hivyo basi kwa kusaini mkataba wa kazi kupitia mfumo huu utaongeza umakini na utekelezaji wa majukumu na malengo.

Naye mkurugenzi wa idara ya utawala na rasilimali watu OR-TAMISEMI Bw. Mohamed Pawaga aliwataka wakuu wa idara na vitengo kuhakikisha wanawapangia majukumu wafanyakazi walio chini yao ili kuleta ufanisi katika utendaji, vilevile alisema kuwa ujazwaji wa OPRAS utafanyika tarehe 1-15 julai kila mwaka.

Hapo awali watumishi wa umma walikuwa wakijaza fomu TFN 743 ambao ulikuwa ni upimaji wa utendaji kazi wa siri na sasa kupitia mfumo huu wa OPRAS watajaza fomu namba 832 ambayo inaruhusu majadiliano baina ya wafanyakazi na wakuu wao wa vitengo na idara huku kukiwa na shuhuda wa kufuatilia makubaliano hayo yanavyofikiwa.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.