Serikali yataka Miradi ya Maji itekelezwe kwa wakati

Enock Mhembano

Serikali yataka Miradi ya Maji itekelezwe kwa wakati

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amewataka wakandarasi kutekeleza miradi wanayopewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa wakati,na kwa uaminifu na kuacha ubabaishaji.

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Wilunze wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Mheshimiwa Jafo amesema mkandarasi yeyote atakayepewa zabuni ya mradi katika halmashauri yoyote nchini na asiitekeleze kwa wakati atambue kuwa hataweza kupewa tenda mahali popote.

Alisema kuwa kumekua na tabia ya ubabaishaji kwa baadhi ya wakandarasi ambapo pindi wanapopewa zabuni ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wamekuwa wakichelewa kuikamilisha, na kuonya kuwa kamwe tabia hiyo Serikali haitaivumilia.

"Kumekuwa na uzembe kwa wakandarasi, mkandarasi anapewa kazi ya kujenga daraja, kujenga visima vya maji, barabara au mradi mwingine wowote katika halmashauri, badala ya kutekeleza mradi huo kwa wakati ili wananchi waendelee kupata huduma hiyo, yeye analeta uzembe na ubabaishaji, mtu wa namna hiyo hatutamvumilia katika serikali hii," alisema Mhe. Jafo.

Aidha amewataka wanakijiji wa Wilunze kuulinda mradi huo wa maji ambapo ametaka kila mkazi wa kijiji hicho anapaswa kuwa msimamizi wa mradi na kuutaka Uongozi wa kijiji hicho kuhakikisha kuwa kinaundwa chombo cha watumiaji wa maji kijijini hapo ili kiusimamie mradi huo.

Mradi wa maji wa kijiji cha Wilunze uliozinduliwa na Naibu Waziri ni moja kati ya miradi ya maji ya vijiji kumi inayojengwa wilayani Chamwino kupitia Programu ya Maji Vijijini. Mradi huo uliojengwa na Mkandarasi M/S Kijima Contractors akisimamiwa na Ofisi ya Mhandisi wa maji wilaya ya Chamwino umegharimu jumla ya sh. 347,909,621.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.