Waziri Simbachawene aagiza tawi la chuo kufungwa

Shani Amanzi na Enock Mhembano

Waziri Simbachawene aagiza tawi la chuo kufungwa

Bodi ya Chuo cha serikali za Mitaa Hombolo imeagizwa kuanza mchakato wa kufunga na kulifuta tawi la chuo hicho lililopo Dodoma mjini kutokana kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mrundikano wa wanafunzi.

Agizo hilo lilitolewa hivi karibuni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhe. George Simbachawene baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika tawi hilo.

Aliagiza wanafunzi wote waliopo katika tawi hilo kurudishwa makao makuu ya chuo hicho Hombolo Nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma.

"Alisema kumekuwepo na matatizo mengi kwenye tawi hilo ambapo kuna wanafunzi zaidi ya 700 huku jengo hilo likiwa na madarasa manne tu na kukosekana kwa viti hali inayowalazimu wanafunzi kutumia viti vya plastiki.

"Kwa mazingira mnayosomea sijaridhishwa nayo kuanzia sasa naagiza Menejimenti ya Chuo, serikali ya wanafunzi na Bodi kwa ujumla muanze mchakato na mazungumzo ya kuona namna gani tunarudi kule Hombolo Main Campus,serikali imejenga majengo mazuri na mengi ya kutosha"amesema

Ametaka mchakato huo uanze kwa muda mfupi na Wizara itatoa maamuzi.

Aidha ameagiza nyumba zinazochukuliwa kwa ajili ya matumizi ya masomo ni vyema zikawa kwenye mazingira ya kuridhisha.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.