Naibu Waziri ahimiza wananchi kujitokeza kupata huduma za afya

Shani Amanzi

Naibu Waziri ahimiza wananchi kujitokeza kupata huduma za afya

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo amewataka Wakazi wa kijiji cha Mvumi na vijiji jirani kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya afya inayotolea na Madaktari bingwa waliotoka katika hospitali mbalimbali nchini kwa kuwa huduma hizo zinapatikana kwa bei nafuu na kutoka kwa Madaktari bingwa wenye uzoefu mkubwa na wa muda mrefu.

Mhe.Jafo ameyasema hayo hivi karibuni wakati alipotembelea hospitali ya Mvumi ambapo amezindua huduma ya Hospitali Kimbizi inayohudumiwa na Madaktari Bingwa ambao watatoa huduma ya kitabibu ndani ya siku tano kuanzia, tarehe 15 hadi Mei 19, 2017.

Madaktari hao bingwa watatibu magonjwa ya ndani kwa watu wote, watoto, mifupa, masikio, pua na koo, meno, upasuaji na magonjwa ya uzazi kwa upande wa akinamama.

Amesema katika sehemu mbalimbali alizopita kumekuwa na changamoto ya kukosa huduma bora katika vituo vya Afya kutokana na urasimu walionao Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na kufanya Wananchi wengi wasio na uwezo wa kupata huduma hizo hivyo, Serikali imeviagiza vituo vya afya kuzitumia vyema pesa za Miradi ya Afya katika kuboresha huduma za Afya kwa Wananchi.

Aidha, amepongeza ushirikiano uliopo wa Mganga Mkuu wa Dodoma, Mbunge wa Jimbo la Mtera, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, wadau mbalimbali pamoja na Kanisa la Anglikana kwa kuweza kuendesha zoezi hilo la huduma.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.