Halmashauri Wilayani Tarime yaagizwa kuwekeza mradi wa miwa

Sylvia Hyera

Halmashauri Wilayani Tarime yaagizwa kuwekeza mradi wa miwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.George Simbachawene (MB) amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mara na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kutekeleza mara moja uwekezaji wa mradi wa kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari Wilaya ya Tarime.

Mhe, Simbachawene alitoa agizo hilo jana mjini Dodoma katika kikao chake na Wenyeviti wa mitaa, Madiwani na Wenyeviti wa Vitongoji kutoka katika kata za Kisaka, Weigita, Bisaru na Matongo kutoka katika Wilaya ya Tarime kuhusu uwekezaji wa mradi wa kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari Wilaya ya Tarime.

Alisema kuwa japokuwa mradi huu unahusisha Wizara nyingi lakini TAMISEMI itajikita kwenye eneo lake ili kuhakikisha mradi huu unaendelea na kutokomeza uzalishwaji wa kilimo cha bangi ambayo inaharibu vijana ambayo ni nguvu kazi ya Taifa na kuleta umaskini nchini.

"Nawaagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tarime na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dtk Mlingwa kuingilia kati na kusimamia uwekezaji huu ili kuhakikisha kwamba mradi huu muhimu na adimu unaanza," alisema.

Aidha Mhe. Waziri aliihoji Halmashauri ya Wilaya ya Tarime juu ya mamlaka yake katika kuingilia mkataba wa uwekezaji wa mradi huu badala ya vijiji hivyo vinne, ambapo alieleza kuwa Halmashauri ni mnufaishaji na kazi yake ni kuhakikisha ya kwamba uwekezaji unakuwa wa tija na sio kuingilia mkataba baina ya muwekezaji na vijiji hivyo vinne.

"Mradi unafanyika kwenye vijiji vinne ambavyo vipo kwenye Halmashauri ya Tarime kwanini Halmashauri iingilie mkataba huu? Kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya Vijiji, vijiji ndivyo vyenye haki ila Halmashauri ina vijiji vyake ambavyo vipo chini yake," alisema

Naye Chacha Getangite Mohabe ambaye ni mwananchi kutoka katika kata ya Matongo amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa kulichukua ombi hilo na kulipitisha kwasababu mradi huo utaleta ajira kwa vijana na kuwafanya wananchi kujikita katika kilimo cha miwa na si bangi kama ilivyokaririwa.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.