Serikali, PS3 kutumia mfumo kupeleka fedha kwenye vituo vya afya

Enock Muhembano na Shani Amanzi

Serikali, PS3 kutumia mfumo kupeleka fedha kwenye vituo vya afya

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Afya Dkt. Zainabu Chaula amewataka wananchi kushirikiana na Serikali katika kutekeleza mpango wa kupeleka fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za Afya nchini.

Dkt. Chaula aliyasema hayo jana mjini Dodoma, wakati wa kikao cha siku tatu kinacholenga kujadili namna ya kutekeleza mpango wa kupeleka fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za Afya ambao kwa kiingereza unajulikana kama Direct Facility Financing –DFF.

Utekelezaji wa mfumo huo unatarajia kuanza mwezi Julai 2017 katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya ambavyo vipo chini ya mikoa 13 inayotekeleza Mradi wa Uboreshaji wa Mifumo katika Sekta ya Umma(Public Sector System Strengthening-PS3).

Mfumo huo unalenga kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ambapo Serikali inashirikiana na katika kuutekeleza.

Dkt Chaula alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha Watumishi wa Afya pamoja na wadau mbalimbali wanapata elimu ya kutosha ya namna ya kutumia mfumo huo ili kuepukana na changamoto za vifaa tiba na huduma zinazokabili Vituo hivyo.

Kwa kuanzia mfumo wa upelekaji fedha moja kwa moja katika vituo vya afya utatekelezwa katika Mikoa 13 na Mamlaka za Serikali za Mitaa 93 ambapo mradi wa PS3 unatekelezwa na mikoa mingine iliyobaki mazungumzo yanaendelea ili kukamilisha shughuli hiyo nchi nzima.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TEHAMA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) bwana Erick Kitali alisema Mifumo ya Tehama inasaidia sana kuboresha utendaji wa kazi na kuondoka kwenye tatizo la kufanya kazi kwa mazoea,na kuongeza uwazi, upataji wa taarifa za mapato na matumizi ya fedha na upatikanaji wa huduma bora kwa wakati.

Bwana Kitali alisema kutakuwa na taarifa za kila kituo kwenye ngazi ya Halmashauri na Wizara pia vituo vya mashirika ya dini vitaingizwa katika mifumo pia kwa kutumia mifumo hadi kwenye ngazi za vituo vya huduma ili kupunguza wingi wa kazi, kupunguza makosa mbalimbali ya uingizaji wa takwimu.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.