Serikali yaipongeza asasi ya TWAWEZA kwa kutoa motisha kwa walimu

Sylvia Hyera

Serikali yaipongeza asasi ya TWAWEZA kwa kutoa motisha kwa walimu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene (MB) amepongeza jitihada zinazofanywa na asasi huru ya Africa Mashariki inayoshughulika na utafiti na uhamasishaji Twaweza katika kutafuta majawabu ya kuinua kiwango cha Elimu nchini.

Waziri Simbachawene alitoa pongezi hizo alipozungumza katika tukio la kuwazawadia walimu waliofundisha vizuri wanafunzi wa darasa la I,II, na III lililoandaliwa na asasi hiyo kupitia majaribio ya kisayansi yajulikanayo kama Kiufunza , jana katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.

Katika Hotuba yake Mhe, Simbachawene aliwapongeza pia kwa kazi nzuri waliyoifanya kupitia utafiti wao wa kuoanisha utoaji wa motisha kama kichocheo cha walimu kuongeza jitihada za kufundisha sambamba na matokeo mazuri

"Malipo kwa walimu baada ya matokeo ni mpango mzuri kabisa , na sikatai kabisa kuwa motisha hii inaweza ikawa kichocheo kwa walimu kufanya vizuri na wanafunzi kufanya jitihada katika kujifunza,"alisema.

Aliongeza kuwa utafiti huu unawapatia wadau na Serikali uwanja wa kutafakari kwa kina ikiwezekana kuangalia namna bora ya kuanza kutekeleza mpango kama huu kwa nchi nzima ili kuleta ustawi wa elimu chini.

Aidha Mhe. Waziri aliwaomba wazazi washirikiane na wadau pamoja na Serikali ili kustawisha elimu nchini kwa kwa kuwatengenezea mazingira rafiki watoto kwasasabu watoto ni hazina sio tu kwa Taifa bali kwa wazazi pia.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Bw.Aidan Eyakuze amewataka walimu wote nchini kuwa na moyo wa kuthubutu na kujifunza kama walimu waliozawadiwa na Asasi hiyo kwa kufundisha vizuri wanafunzi katika shule zao.

Twaweza ni asasi huru ya Afrika Mashariki inayoshughulika na utafiti na kuhamasisha Umma kuchukua hatua ili kuendeleza sekta ya elimu nchini.Asasi hii inafanya kazi kwa kushirikiana na Serikali kutafuta njia za kuboresha kujifunza chini yaa jaribio la kisayansi lijulikanalo kama Kifunza lililozinduliwa na Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Seriklai za Mitaa (TAMISEMI) ,Mh. Hawa Ghasia (Mb) mwezi januari 2013

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.