Watahiniwa Kidato cha sita waaswa kutojihusisha na udanganyifu

Enock Ernest

Watahiniwa Kidato cha sita waaswa kutojihusisha na udanganyifu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR- TAMISEMI), Mh. George Simbachawene amewaasa watahiniwa wa kidato cha sita kufanya mitihani yao kwa kuzingatia kanuni na taratibu na kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2017 nchini, jana ofisini kwake mjini Dodoma, Waziri Simbachawene alisema, mtihani wa kidato cha sita umeanza tarehe 02/04/2017 na unatarajiwa kumalizika tarehe 19/05/2017.

Vilevile, Mheshimiwa Simbachawene aliongeza kuwa maandalizi yote tayari yamekwishafanyika hivyo mitihani itafanyika kwa amani, utulivu na pia usalama katika vituo vyote ni wa kutosha kwa kuzingatia kanuni na taratibu za baraza la mitihani Tanzania.

Aidha amewataka viongozi wote na wasimamizi katika ngazi za mikoa, wilaya halmashauri na vituo waendelee kusimamia mitihani hiyo kwa weledi, uaminifu, uadilifu na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa watahiniwa.

Wakati huo huo Mheshimiwa Simbachawene amewatakia watahiniwa wote wa mtihani huo afya njema na baraka tele na mafanikio makubwa katika mtihani wao.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.