Serikali yaahidi kuboresha maslahi ya watumishi wake

Shani Amanzi

Serikali yaahidi kuboresha maslahi ya watumishi wake

Serikali imeahidi kushughulikia kero mbalimbali zinazowagusa Wafanyakazi zikiwemo malipo kidogo ya mshahara, ushirikwishaji hafifu katika mabaraza ya Wafanyakazi, madeni sugu ya Wafanyakazi, pamoja na makato makubwa ya kodi ya mapato.

Aidha Serikali inanuia kuboresha kiwango cha fedha kinachotoa kwa wanafunzi kupitia bodi ya mikopo Elimu ya juu na ombi la kupunguziwa gharama za mauzo ya nyumba na viwanja.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jabiri Shekimweri ameyasema hayo hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani Mei Mosi yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania mjini Dodoma.

Alisema kuwa kwa kuwa Serikali ya Tanzania ni Mwanachama wa Shirika la Kazi duniani inatambua na kuthamini utu wa Wafanyakazi na iliridhia Mikataba mingi yenye kulinda haki za Wafanyakazi.

"Napenda kuwahakikishia Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Wafanyakazi kupitia TUCTA ikiwemo kuridhia Mikataba mengine ambayo inamanufaa kwa Taifa na Wafanyakazi kwa ujumla," alisema

Kwa upande wa Mishahara, Mheshimiwa Shekimweri amesema Serikali inaandaa utaratibu wa kuboresha Mishahara ya Watumishi wa Umma baada ya kukamilisha zoezi zima la uhakiki na Wafanyakazi na wanaombwa kuwa wavumilivu wakati Serikali inaendelea kukamilisha taratibu na baadae kupeleka kwenye vyombo husika.

Pia kumekuwa na malalamiko ya Sekta binafsi kutowapa Wafanyakazi Mishahara wanayostahili na Mikataba hivyo basi kwa Watumishi wa Sekta binafsi bodi iliyoundwa itatoa kima cha chini hivi karibuni nakupeleka mapendekezo yake kwa Serikali baada ya kufanya uchambuzi wa kiwango kinachostahili.

"Serikali inapenda kuona Wafanyakazi wanapata ajira yenye staha lakini mkumbuke kuwa uwezo wa kulipa Mshahara mzuri unatokana na Kampuni,Taasisi au Serikali kuwa na kiwango kizuri cha uchumi na Tanzania imekuwa ikitekeleza sera mbalimbali kwa lengo la kukuza uchumi hatua ambayo itafikiwa tu kama jamii itafanya kazi zenye kuongeza mapato na kusimamia ukusanyaji wa kodi kikamilifu," alisema.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.