Wazazi watakaoshindwa kupeleka watoto shule kuchukuliwa hatua

Na Fred Kibano

Serikali kuanzisha Wakala wa Barabara Vijijini

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa I. Iyombe amewataka Wadau wa barabara waliohudhuria kikao cha kazi kuhusu Wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) “Rural and Urban Roads Agency” kuchangia kwa kutoa mawazo ambayo yatapelekea ufanisi wa huduma za barabara za Mamlaka za Serikali Mitaa na utatuzi wa changamoto zilizopo.

Mhandisi Iyombe amesema matarajio ni kupata mawazo chanya yatakayosaidia kuwa na chombo ambacho kitaondoa matatizo yaliyopo kwa hivi sasa kama ufanisi mbovu wa huduma za barabara hizo, ucheleweshwaji wa michakato ya manunuzi, ucheleweshwaji wa kuanza kazi za barabara, mipango mibovu, usimamizi mbaya, changamoto za kifedha na kutoonekena kwa thamani ya barabara hizo.

Akiongea kwa niaba ya Serikali wakati wa kikao cha kazi jijini Dar es Salaam, katika kikao cha kilichowahusisha baadhi ya Wahandisi na Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Ujenzi, Mikoa, na Wadau wa Maendeleo na baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa Mhandisi Iyombe amesisitiza kutofanya kazi kwa mazoea kwani Serikali ina moyo wa dhati na nia njema ya kuwatumikia Watanzania kwa kujenga uchumi na kuondoa umasikini kama inavyoeleza Ilani ya Chama Tawala.

Aidha, amesema Wakala mpya TARURA baada ya kukamilika inatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika sekta ya barabara nchini na kutekelezwa kwa mujibu wa Ilani ya Chama Tawala.

Kwa upande wake Mhandisi Elina Kayanda Mkurugenzi wa Idara ya Miundo mbinu TAMISEMI amesema uanzishwaji wa Wakala wa barabara Mijini na Vijijini kutasaidia kutoa huduma bora kwa Watanzania kwa kuendeleza, kutengeneza na kurahisisha mawasiliano baina ya miji na vijiji. Lakini pia kushughulikia masuala ya ukimwi, utawala bora, usawa wa kijinsia na masuala ya mazingira.

Mhandisi Kayanda amesema kipindi cha kwanza cha utendaji wa Wakala kinatarajiwa kuwa miaka mitano kuanzia 2017/18 mpaka 2021/2022

Akihitimisha mada aliyotoa kwa Wadau hao, Mhandisi Kayanda amesema Muundo wa Wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) unatarajiwa kuwa na Idara tano za Maendeleo ya Miji na Matengenezo, Maendeleo vijijini, Mipango na Msaada wa Kiufundi na pia Msaada wa Huduma za Kibiashara kwa upande wa vitengo vinne ni Manunuzi, Msaada wa kisheria, ukaguzi wa ndani na pia kitengo cha Fedha na Uhasibu.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.