erikali kuboresha mfuko wa afya ya jamii kwa Wananchi wote

Na.Fred Kibano

Serikali kuboresha mfuko wa afya ya jamii kwa wananchi wote

Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula amewataka Watendaji wa Serikali pamoja na Wadau wote kutekeleza maboresho ya huduma za afya nchini hususani Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

Dkt Zainab Chaula ameyasema hayo wakati wa kikao cha watendaji toka Menejimenti ya Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Wizara ya Afya na Watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambapo mada kuu ilikuwa Muundo na Utekelezaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii Ulioboreshwa (Universal Health Coverage – UHC).

Dkt Zainab Chaula amesisitiza kuondoka katika utendaji wa mazoea na kuwa wa kivitendo zaidi kama yalivyo matarajio yanayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya tano, ‘’tutoke kwenye majaribio twende kwa vitendo, matarajio ya miundo mbinu yanatakiwa kufanyika ndani ya miezi miwili kwani huduma za kiafya kwa wananchi bado zipo duni ndiyo maana wananchi wanazikimbia zahanati’’.

Amesisitiza kuwa watu wote wanahitaji huduma ya bima ya Afya na siyo vijijini pekee ijapo kuwa ndipo kwenye mahitaji makubwa, “kwa mwananchi wa kawaida ni tatizo kubwa, ni lazima tujipange, tubadilike na twende kielektronic mfano hai pale unaposahau kitambulisho cha Bima ya Afya nyumbani” Aidha, amekataa mpango wa kuanzia halmashauri 50 na badala yake uanze katika halmashauri zote 173 nchini.

Akiwasilisha mada ya Muundo na Utekelezaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii Bw.Bernad Konga ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya amesema lengo la maboresho ya Mfuko huo ni kuhakikisha sheria ya afya bora kwa wote (Universal Health Coverage) inafanikiwa na kwamba timu ya Wataalam iliyoshirikisha wadau wake imekwisha tengeneza muundo wa Mfuko wa jamii (CHF),masuala ya usimamizi mzuri katika halmashauri, uwekaji wa Mifumo ya teknolojia ya habari na kuboresha upatikanaji wa dawa.

Bw.Konga amesema kuwa, Mfuko wa bima ya Afya ya Jamii kwa hivi sasa una changamoto ya upatikanaji wa dawa, ukomo wa kupata dawa, muundo wake, pia usimamizi na uendeshaji. Matarajio yake ni kuondoa kero zote na kuwa na huduma bora ya afya kwa Watanzania wote.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.