• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Waziri Jafo: Tutaendelea kufanyakazi kwa kasi

Imewekwa tar.: December 10th, 2020


Na. Angela Msimbira DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo amesema kwa sasa TAMISEMI  itafanyakazi  kwa kasi   ya  kushambulia na kufuatilia ili kufukia mapungufu yaliyopo  katika utendaji kazi.

Akiongea na Menejimenti ya Ofisi hiyo leo  Jafo amewataka watumishi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi hasa katika kutoa huduma kwa jamii ili kupunguza kero mbalimbali zinazotolewa na wananchi

Amewataka watumishi wote kujenga mahusinao mazuri katika kazi ili kuleta mabadiliko kwa jamii na kufikia malengo ya Serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akiongelea kuhusu  Sekta ya Elimu  Waziri Jafo amemuagiza katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga kuandaa taarifa itakayoonyesha  matumizi  ya fedha  zilitolewa  mnamo tarehe  26/6/2020  kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni, Madarasa ili kujua maeneo yaliyokamilisha ujenzi huo na wale  ambao hawajakamilisha, na nini  mikakati ya kukamilisha.

Amewataka watendaji wote nchini kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo ikiwemo fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu  ili fedha zitakazotumika ziendane na majengo yanayonjengwa

Hata hivyo, amemuagiza Katibu Mkuu huyo kuhakikisha  wanapata taarifa  ya mikakati ya Mikoa kuhusu ujenzi wa madarasa ili kuhakikisha watoto wote waliofaulu mitihani ya kumaliza elimu ya msingi wanapata nafasi  ya kuendelea na masomo

Waziri Jafo amewataka viongozi wa Sekta ya Afya na TARURA kuhakikisha wanapanga mikakati madhuburi ya kuainisha vipaombele vya Serikali katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Amewataka TARURA kuhakikisha  wanasimamia kwa karibu  miradi inayotekelezwa na kuacha  kuwatumia  wakandarasi wanaojifanya  kujulikana  na  wanamiradi mingi ya kufanya na kuwataka kuhakikisha  miradi yote iliyopo  chini ya TAMISEMI  inakamilika kwa wakati uliopangwa

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya   Mhe Festo Dugange  amesema pamoja na ruzuku za Serikali tutaendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vya kutolea huduma, ili  kuhakikisha fedha zinazokusanywa katika vituo vya kutolea huduma za afya zinapelekwa katika  kuboresha huduma za afya, upatikanaji wa dawa na vitendanishi matengenezo madogomadogo na hatimaye kuendelea kwa hatua kupunguza utegemezi  kwa bajeti ya Serikali

Wakati huohuo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Mhe. David Silinde amesema kuwa wamekuja kuongeza ufanisi wa utendajikazi, kuhakikisha kuwa huduma inawafikia wananchi moja kwa moja.

Aidha amewataka watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuacha kufanyakazi kwa mazoea bali watumie mazoea na uzoefu walionao ili kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa wananchi’



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Vikundi 47 Kondoa vyapewa mikopo ya shilingi milioni 147

    February 24, 2021
  • Mikopo ya Shilingi Milioni 85 yatolewa kwa Vikundi wilayani Bunda

    February 24, 2021
  • Mradi wa Fursa na Vikwazo Iliyoboreshwa Kuingizwa kwenye Majukumu ya OR - TAMISEMI

    February 23, 2021
  • Mikopo ya Sh. Milioni 850 yatolewa kwa Vikundi 104 jijini Tanga

    February 15, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.