• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Waziri Jafo Awaaga wana OR TAMISEMI

Imewekwa tar.: August 21st, 2020

Na Fred Kibano

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Selemani Jafo amewashukuru wanafamilia ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kumpa ushirikiano mzuri kipindi alichohudumu katika wizara hiyo.

Waziri Jafo ameongea katika hafla fupi ya chakula cha jioni aliyoiandaa binafsi kwa ajili ya kuwaaga Viongozi na watumishi wa wizara hiyo huku akisema ushirikiano mkubwa ndio chanzo cha yeye kuhudumu mpaka hatua aliyofikia hali akimsaidia Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

“nakushukuru sana Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Nyamhanga na timu yako mmekuwa mstari wa mbele katika kunisaidia kwenye majukumu mbalimbali ambayo nimeyatekeleza katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa”

Jafo amesema wizara hiyo ambayo ina majukumu lukuki ni wizara ngumu na yenye matatizo mengi kwani inahusu maisha ya kila siku ya Watanzania na hanabudi kuwashukuru Viongozi wa wizara hiyo na watumishi ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yake bila hata kujali umri wao.

“wengi hamkujalisha umri wenu wakati mkifanya kazi nami, pia madaraka niliyopewa na Mhe. Rais nikiwa kijana mmdogo, kazi tuliyoifanya katika miaka mitano ni kazi kubwa sana na huwezi kupata mafanikio kama huna timu work (timu ya kufanya kazi pamoja)”,alisema Jafo.

Aidha amesema anaendelea na mchakato wa kuomba ridhaa kwa watanzania ambao watampigia kura kuwa mbunge waa Kisarawe lakini yeye binafsi angependelea kuendelea na wizara hii ambayo amepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Watendaji na watumishi na hivyo kama akipewa nafasi ya kuingia katika Baraza la Mawaziri na na kama ikimpendeza Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amrudishe katika wizara hiyo ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Katibu Mkuu Ofisi yaRais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amemshukuru kwa kualikwa wanafamilia wa ofisi yake na kwamba ofisi hiyo wiki mbili zilizopita iliadhimisha  wiki ya Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kuonyesha mafanikio ya sekta ya Afya, Elimu, Miundombinu ambayo waziri Jafo amekuwa chachu ya mafanikio hayo.

Mhandisi Nyamhanga amesema angependa waziri Jafo arudi katika wizara hii lakini jambo hilo hana mamlaka nalo lakini pia kama hatorudi basi maombi yake ni kupata nafasi kubwa zaidi.

“Jafo ana maono ya mbali na usipokuwa makini atakuacha mbali sana tumekuwa na mafanikio makubwa chini ya uongozi wake, pongezi pia natoa kwa Mheshimiwa Mwita Waitara na Mheshimiwa Josephat Kandege kwa kushind kura za maoni kwenye majimbo yao ya uchaguzi na kuteuliwa na chama kugombea ubunge”

Aidha, Nyamhanga amesema Mhe. Jafo atakuwa jimboni mwake kwa muda mrefu na kwamba cheo chake cha uwaziri kitaendelea kuwepo mpaka masaa machache ya kuapishwa kwa Rais Mteule baada ya kutangazwa matokeo.

Kwa upande wake Bwana Tixon Nzunda Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ameshukuru Mhe. Jafo kwa kuonyesha upendo na kuwaleta pamoja wanafamilia ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na kuwa amejifunza mambo mengi kutoka kwake.

“wewe ni mtu mwemwa sana na kama kufanya kazi kama timu wakati wote ulituleta pamoja wana TAMISEMI pamoja na Viongozi wengine na kuamini kuwa kila mmoja ana mchango katika taasisi, niseme tu Mheshimiwa Waziri unayo bidii ya kazi, unaonekana mdogo lakini unafikiria mambo makubwa kwa wizara hii na umejenga heshima kubwa kwako na Watanzania”

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Kessy Maduka amesema kwamba tangu alipokuwa Waziri amewaunganisha watu wote na kuwakomaza kwa kuwapa matumaini na kuwafanya  kuwa watendaji.

Winfrida Rutaindurwa Katibu Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) amemsimulia Jafo kama mtendaji ambaye hataki Viongozi kukaa maofisini bali kwenda maeneo ya kazi na kufanya ufuatiliaji wa kina ili kupata matokeo.

“namkumbuka waziri Jafo pale aliposema, msikae ofisini bali nendeni sight (maeneo ya kazi) mkajionee na kufanya kazi huko, pia bajeti ya Tume ya TSC imepanda sana kwa kuipigania na inasaidia uendeshaji wa ofisi yetu ukilinganisha na kipindi kilichopita, tunatoa pongezi pia kwa ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jengo limejengwa vizuri”

Akitoa neon la shukrani Asifiwe Makweta ambaye ni Afisa Tawala Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema, “katika utendaji wako wa kazi umesisitiza kufanya kazi kwa weledi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea, tumeweza kufanya wizara mpya kupitia wewe, umefanya TAMISEMI kujulikana sana”

Katika hafla hiyo walihudhuria Viongozi wa wizara, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambazo ni Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa, DART, Chuo cha Serikali za mitaa Hombolo, Shirika la Masoko Kariakoo, Shirika la Elimu Kibaha na TARURA.


Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.