• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Book History
    • Kuhusu Wizara
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Utawala
    • Directory
    • Vitengo
    • Muundo wa Wizara
    • Mikoa, Wilaya na Halmashauri
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji

Wataalamu TEHAMA Wapewa siku 90 kukamilisha Mfumo wa GoTHOMIS

Imewekwa tar.: November 13th, 2019

Wataalamu wa TEHAMA, kutoka Wizara ya Afya, OR-TAMISEMI, Wakala ya Serikali Mtandao na Wizara ya fedha wamepewa  miezi mitatu kukamilisha maboresho ya mfumo wa GoTHOMIS ambao unatumika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa ngazi ya Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya  pamoja na zile za Rufaa za Mikoa.

Agizo hilo limetolewa kwa Nyakati tofauti na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainabu Chaula pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima, waliopo watembelea wataalamu hao ili kutaka kujua hatua waliyofikia na mustakabali wa ukamilishaji wa kazi hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara yake iliyofanyika mapema siku ya Jumapili Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI mara baada yakupokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa TEHAMA OR-TAMISEMI, Erick Kitali alisema ni vema kazi hiyo ika kamilika kwa wakati ili Mfumo uweze kufanya kazi na kurahisisha mambo mengi ambayo yamekuwa yakienda ndivyo sivyo.

“Mkurugenzi Erick ametumbia hapa kazi hii itakamilika mwezi Machi, 2020 naomba mkamilishe kama mlivyosema tafadhali” alisema Dkt. Gwajima na kuongeza “Nitumie fursa hii kuwaagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri kuanza sasa maandalizi ya ununuzi wa Komputa kwakuwa gharama zake hazidi milioni 1.5, nawaomba na wao waanze  kwa kununua hata komputa moja moja kupitia mapato ya ndani ili mfumo utakapo kamilika tu waanze kazi mara moja.” Alisisitiza Gwajima.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee, Watoto na Watu wenye Ulemavu Dkt. Zainabu Chaula, yeye wakati wa ziara yake mara baada yakupokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo alisema muda waliojiwekea ni mkubwa hivyo angependa kuona kazi hiyo inakamilika ndani ya miezi mitatu.

“Mmesema Mfumo utakamilika mwezi machi, 2020, nadhani muda huu mlioweka ni mwingi mno, sasa mimi naagiza ndani ya miezi miwili muwe mmekamilisha na mimi nitafanya ufatiliaji” alisema Dkt. Chaula

Dkt. Chaula alisema kwamba, mbali na kuwapa siku tisini kukamilisha zoezi hilo lakini pia amewataka kutambua ijtihada za wataalamu wazawa ambao ndio waliuasisi mfumo wa GoTHOMIS.

“Kaaya hivi yuko wapi, tunapasema tutembee pamoja, lazima tuwatambue na kwenda nao watu kama hawa, kazi kubwa aliyoifanya mtu huyu atafutwe na tumshirikishe kwani yeye si IT specialist kama nyie”? Alisema Dkt. Chaula na kuhoji.  

Awali wakitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la uboreshaji wa mfumo huo, Wakurugenzi wa TEHAMA Erick Kitali wa OR-TAMISEMI na Haji Bamsi wa Wizara ya Afya waliwaambia viongozi hao kuwa katika mazingira ya sasa mfumo utagawanyika katika sehemu tatu kuu ambazo GoTHOMISI Lite, standards na Specialized

Erick Kitali alisema, GOTHOMIS Lite, itaweza kutumika katika ngazi ya zahanati na itaweza kutumika teknolojia kama POS au simu za kiganjani ambazo hata miundominu yake ni kazi kufikika kwa sasa wakati, toleo la GOTHOMIS Standard imelenga kutumika na vituo vya afya na hospitali za rufaa zaidi sana toleo litaweza kubadilishana taarifa na mifumo mingine muhimu kama DHIS2, eLMIS na GOTHOMIS Specialized hili nit oleo maalumu kwa ajili ya hospitali za kitaifa kama Muhimbili ambazo hutoa huduma za vertical programs na specialized clinics,”alisema Kitali.


Mfumo wa GoTHOMIS, kwa hivi sasa katika toleo lililotangulia ulishafungwa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya zaidi ya 400 na hivi sasa unafanyiwa maboresho makubwa ili uwe madhubuti na wenye tija kubwa kwa taifa.

Na Atley Kuni- TAMISEMI, Dodoma.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUWAREJESHA WAGOMBEA WASIO NA MAKOSA YA KIKANUNI KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019 November 10, 2019
  • MAELEZO KUHUSU ZOEZI LA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU ZA MAOMBI YA UTEUZI WA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI October 30, 2019
  • TANGAZO NA ORODHA YA WALIOITWA AJIRA ZA MKATABA TAASISI YA BENJAMIN MKAPA October 25, 2019
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA YA AFYA REPLACEMENT October 25, 2019
  • Orodha ya Majina ya watumishi wa Ajira Mpya kada ya Afya September 18, 2019
  • Muongozo wa Uchaguzi wa Viongozi wa ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa September 06, 2019
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Jafo atangaza waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza, 2020

    December 05, 2019
  • Jafo ambana Mkandarasi SKOIL Building Contractors Limited

    December 04, 2019
  • Jafo akagua ujenzi wa hospitali ya Uhuru

    December 04, 2019
  • Halmashauri zapigwa marufuku kukopa Benki

    November 29, 2019
  • Angalia zote

Video

Rais Dkt. John Pombe Magufuli Dodoma
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.