• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Wasichana wote waliofaulu kidato cha Nne kujiunga kidato cha Tano,Vyuo vya Ufundi

Imewekwa tar.: June 1st, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema wasichana wote waliofaulu katika mtihani wa kidato cha Nne katika mwaka uliopita wa 2018 wamefanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo mbali mbali vya ufundi nchini.

Jafo, ametoa kauli hiyo hii leo mjini Dodoma wakati akitangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi kwa mwaka wa masomo utakao anza mapema mwezi Julai, 2019.

“Nipende kuwatangazia habari njema kuwa, kwa mwaka huu wasichana wote waliofaulu wamefanikiwa kuchaguliwa kujiunga kidato cha tano pamoja na vyuo mbali mbali vya ufundi, ambapo jumla yao ni wasichana 45,816.

Akitoa takwimu za ufaulu wa watahiniwa wa kidato cha Nne kwa mwaka 2018, kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu, alisema ni watahiniwa 113,825 kati yao wasichana ni 47, 779 na wavulana 66,046 sawa na asilimia 31.76 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo, amezitaka Halmashauri hususan ni zenye tahasusi za masomo ya Sayansi na Hisabati kukamilisha madarasa ya kidato cha tano na sita ifikapo Machi, 2020, amezitaja Halmashauri hizo kuwa ni  Kyerwa DC, Kilindi DC, Kilombero DC, Handeni DC, Malinyi, Mtwara DC, Momba DC, Nanyumbu DC na Nanyamba DC, huku akiwataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia kwa karibu na kuhakikisha azma ya Serikali kwa kila Tarafa inakuwa na shule ya kidato cha tano inatimia.

Mwisho Waziri Jafo, amewataka Wanafunzi wote waliochaguliwa kuzingatia maelekezo yote muhimu ikiwepo kuthibisha kuripoti katika shule na vyuo walivyopangiwa kabla ya tarehe ya mwisho hususan kwa wale watakao jiunga na vyuo vinavyo simamiwa na (NACTE).

“Tumetoa tarehe kuanzia 09 Juni hadi 30 Agosti, 2019 wote wawe wamethibithisha kujiunga katika vyuo vya ufundi na watakaoshindwa kufanya hivyo nafasi zao zitajazwa na wanafunzi wengine.” Alisema Waziri Jafo.

Ofisi ya Rais TAMISEMI, imekasimiwa jukumu lakusimamia zoezi la uchaguzi na upangaji wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi kuanzia mwaka 2014 zoezi ambalo huanza kutekelezwa  mara tu baada ya kutangazwa kwa Matokeo ya kidato cha Nne.

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

    January 22, 2021
  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.