• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Wanawake nchini watakiwa kudumisha umoja na upendo katika jamii

Imewekwa tar.: March 8th, 2019

Wanawake nchini wametakiwa kudumisha umoja  na upendo baina yao ili  kufikia mafanikio na maendeleo ya kuinua uchumi  mwaamke wa kitanzania.

Hayo yamebainishwa na  Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi,, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde kwenye  maadhimisho ya siku ya Wanawake  duniani iliyofanyika leo Kimkoa katika viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma.

Mhe. Mavunde amesema kuwa wakinamama wakidumisha umoja na mshikamano wataleta chachu katika kupigania haki za mwanamke na kuleta fikra pevu ndani ya jamii ya kitanzania.

Ameendelea kusema kuwa  wanawake wanatakiwa kuwa na malengo makubwa zaidi bila kusahau majukum yao katika ngazi ya familia  kwa kuwa wao ndio  kiungo muhimu katika malezi, maendeleo na mafanikio ndani ya  jamii.

Naye Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt.  Dorothy Gwajima amesema kuwa wanawake wanatakiwa kuwa na udhubutu katika ngazi yeyote ile anayopangiwa kimadaraka japo kuna changamoto mbalimbali katika jamii lakini wanahitajika kuwa  jasiri katika kufikia malengo na kuleta maendeleo  kwa kuanzia ngazi ya familia,  jamii na taifa kwa ujumla.

“Ili mwanamke aweze kudhubutu lazima  apatiwe elimu itakayomuwezesha  kufanikisha malengo yake aliyojiwekea katika jamii, hasa ukizingatia kuwa mwanamke ndio muhimili mkuu kuanzia ngazi ya familia, jamii  na Taifa kwa ujumla katika  kuleta maendeleo endelevu. ” Amesema Dkt. Gwajima

Dkt Gwajima ameongeza kuwa mwanamke akijitambua katika  nafasi yake kwenye jamii  basi hicho ni kiashiria  tosha kinachoonyesha kuwa yeye  ni jasiri na anawezaa  kusimama na kupewa haki sawa bila kubaguliwa katika jamii inayomzunguka.

Amesema kuwa  katika kutafakari maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inapaswa kutafakari changamoto na mafanikio yaliyokwishapatikana tangu maadhimisho hayo yalipoanza kufanyika kwa kuwa na takwimu sahihi zinazoonyesha mafanikio yaliyopatikana kwa wananwake na jamii kwa ujumla.

Dkt. Gwajima  ameendelea kufafanua ni vyema  mabadiliko ya fikra yakaanzia  ngazi ya Menejimenti  mbalimbali za Serikali kwa kuchambua sera zilizopo  katika kuleta usawa ndani ya jamii na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais,TAMISEMI Bi.Rose Makange ametoa wito kwa wanawake wote nchini  kutumia vikundi vya wanawake vizuri ili kuwa na mafanikio endelevu.

“Wanawake wanatakiwa  kubadili fikra zao kwa kudumisha upendo na mshikamano  ili mwanamke wa kitanzania aweze kusimama imara na kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi  yetu” Amesema Bi. Makange.

Ameongezea kuwa umefika wakati wanawake  kupitia vikundi vyao kubuni nini kifanyike katika kukuza pato la kikundi kwa kuanzisha miradi mbali mbali itakayo kuja kuwasaidia na kuwaletea maendeleo endelevu ndani ya jamii.

Aidha Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani huadhimishwa kila tarehe 8 Machi kila mwaka ambapo  wanawake wote duniani uazimisha siku hiyo ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamefanyika kila Mkoa na Kaulimbinu ya mwaka huu ni “Badili fikra kufikia usawa wa jinsia kwa maendeleo endelevu.



Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Viongozi TBA Kigoma matatani kwa kushindwa kukamilisha miradi

    January 18, 2021
  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.