• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Wananchi watakiwa kushiriki usimamizi huduma za afya.

Imewekwa tar.: April 5th, 2019

Naibu Katibu Mkuu Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt Dorothy Gwajima ametoa wito kwa Wananchi kuimarisha ushiriki wao kwenye Kamati za Usimamizi wa Huduma za Afya katika Vituo vya Kutolea huduma za Afya.

Akihojiwa hivi karibuni kuhusu maboresho ya huduma za afya nchini Dkt. Gwajima amesema, pamoja na kukamilika kwa vituo 352 vilivyozinduliwa  na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jon Pombe Magufuli  Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya afya ambapo kufikia Juni, 2019 awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali 67 za Halmashauri utakuwa umekamilika kupitia mpango wa ushirikishwaji wa Wadau, Wananchi na Serikali kwa ujumla.

Dkt. Gwajima amesema, ushiriki wa Wananchi katika Kamati hizi ni muhimu ili, kuwezesha kuwa na sauti katika mipango ya maendeleo ya vituo husika na utawezesha mipango ya maendeleo ya huduma za afya katika vituo husika kugusa kwa karibu zaidi matarajio yao.

Amesema sambamba na kuboresha miundombinu na kuongeza idadi ya vituo, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa itahakikisha huduma bora zinapatikana muda wote na kufikia matarajio ya watumiaji.

Dkt. Gwajima anafafanua kuwa, azma ya Serikali ni kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana ngazi ya afya ya msingi na kuwapunguzia mzigo wa gharama za muda na fedha Wananchi wenye uhitaji.

“ Upatikanaji wa huduma bora karibu zaidi na Wananchi utawapunguzia gharama za kwenda mbali na makazi yao kufuata huduma ambazo, zinaweza kupatikana katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali za Halmashauri” Anasisitiza Dkt. Gwajima.

Ametoa wito kwa Wananchi kuhakikisha wanawakilishwa vema katika Kamati za Usimamizi wa Huduma za Afya katika Vituo husika kuanzia ngazi ya Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali za Halmashauri

 “Kamati za Usimamizi Huduma za Afya zenye uwakilishi wa Wananchi zishirikiane  na Wataalamu wanaotoa huduma katika vituo husika ili, ushirikiano uendelee katika maendeleo ya huduma za afya na kuwafanya Wananchi kuwa na sauti katika maendeleo husika” Amesema Dkt. Gwajima

Ameongeza kuwa, ni wajibu wa Wenyeviti wa Kamati za Usimamizi wa Huduma za Afya kuwa daraja kati ya kituo husika na Wananchi ili, kuendeleza kuimarisha umoja na ushirikiano katika kuleta maendeleo ya huduma za afya nchini.

Hata hivyo Dkt.Gwajima amewakumbusha watoa huduma za afya nchini  kuwa, mteja ni mfalme hivyo siku zote utoaji wa huduma uzingatie huduma bora kwa mteja ili, Wananchi waendelee kuhamasika kuchangia katika maendeleo ya sekta ya afya.

Dkt Gwajima amesema, pamoja na uwepo wa vituo hivi, Serikali itaendelea kuratibu huduma za tiba kwa mkoba kwa kutumia Wataalamu toka hospitali za kibingwa ili, kuwafikia Wananchi karibu na makazi yao.

Aidha, Dkt Gwajima ametoa Shukrani kwa Wadau wote, Wananchi na Viongozi wote waliosimamia utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa vituo 352 vya kutolea huduma za afya na kuwaomba kuendelea na ushirikiano na mshikamano huu daima.

Na. Angela Msimbira - Masasi Mtwara



Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Mweli awatega Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu kwenye Mfumo wa PREM/PREMS.

    January 10, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.