• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Wananchi waipongeza Serikali kwa kujenga Vituo vya afya wataka huduma ziboreshwe.

Imewekwa tar.: July 30th, 2019

Wananchi wa Kijiji cha Mpwayungu  kata ya Mpwayungu,  Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma  wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  kwa kuwajengea  miundombinu ya afya  ambayo imesaidia kuboresha huduma za afya  katika kijiji hicho.

 Wakiongea leo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya afya na hali ya utoaji wa huduma  za afya katika kijiji hicho iliyofanywa na   Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima wananchi hao wamesema, kabla ya kujengewa miundombinu ya afya hali ya utoaji wa huduma za afya ilikuwa mbaya kiasi ambacho walikuwa wakifuata huduma hiyo katika Hospitali ya Mvumi

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Kituo cha Afya cha Mpwayungu Bw. Chibwele Magubika amesema, awali hali ya utoaji wa huduma za afya katika kituo hicho zilikuwa duni kiasi ya kwamba wananchi wengi walikuwa wakikimbilia kupata huduma hizo katika Hospitali ya Misheni Mvumi au Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Bw. Magubika ameishukuru Serikali kwa kujenga miundombinu ya afya na kuboresha huduma za afya kwa wananchi ila ameiomba Serikali ihakikishe huduma hizo zinaboreshwa na kwamba, watumishi wanakuwa na lugha nzuri kwa wateja na kufanya kazi kwa weledi ili wananchi wengi waweze kuvutiwa na utoaji wa huduma katika kituo hicho.

 “Inasikitisha kuona Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa  miundombinu ya afya yakiwemo majengo mazuri makubwa na yenye kuvutia lakini baadhi ya watumishi bado wanakuwa na lugha chafu ambazo haziwavutii wananchi kuja kupata huduma kwenye vituo kama hivi” Amesema Magubika.

Ameendelea kufafanua kuwa kuna baadhi ya watumishi hapa ni watovu wa nidhamu, wana lugha chafu kabisa, hawana maadili katika utendaji kazi wao, wanalewa pombe, hawatoi huduma kwa wakati jambo ambalo linakatisha tamaa wananchi kufika kupata huduma.

Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mpwayungu Selemani Kibakaya amesema kuwa, huduma zikiboreshwa, watumishi wakafanya kazi kwa ushirikiano bila kutegeana itasaidia kupunguza changamoto mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi,

Amewataka wafanyakazi kuhakikisha wanatoa huduma kwa wakati, kwa kuwajali wagonjwa ili kuweza kupunguza msongamano pamoja na wananchi kukaa muda mrefu kusubiri huduma za afya jambo ambalo linakatisha tamaa ya kupata huduma za afya.

Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima amawaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanafanya ufuatiliaji wa kero wanazopata wananchi wakati wa kufika kwenye vituo vya huduma kwa kuongea na wateja, viongozi wa serikali ya kijiji na Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Kituo wanaowawakilisha wananchi kwenye uongozi wa kituo.

Vilevile, Dkt, Gwajima amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanachukua hatua stahiki kwa wakati pale wanapopelekewa malalamiko siyo tena nao wanakaa miezi 6 bila kuchukua hatua kama ilivyotokea kituoni hapo.

Dkt Gwajima amesema, ukosefu wa hatua stahiki dhidi ya kero zinazoripotiwa na wananchi ndiyo mojawapo ya mambo yanayowakwaza wananchi na kuamua kutotumia vituo husika au kuamua wanavyoona wao inafaa.

 “CHMT NA RHMT hakikisheni mnafuatilia na kusimamia  utendaji kazi wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma, kutoa msaada na ushauri wa kitaalamu pia, kusikiliza kero za wananchi dhidi ya huduma na katika kila jambo, kuchukua hatua stahiki kwa wakati na bila kuonea upande wowote ule. Msisubiri hadi Wizara itembelee ndiyo iibue hizi kero na nyie mpo huku.

Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kuhakikisha anafanyia kazi malalamiko ya wananchi na kuchukua hatua stahiki za kiutumishi dhidi ya mtumishi Claude Chilala ambaye anatuhumiwa na wananchi kukiuka maadili ya kiutumishi na kuwa kero sugu kwa wateja.

Dkt. Gwajima amewapongeza watumishi wengine ambao wananchi wamekiri kuwa hawana shida ukilinganisha na huyo anayelalamikiwa na kila mteja.

Aidha amewataka watumishi kutoiga tabia ambazo zinakiuka maadili ya utumishi wa umma na kwamba, washirikiane daima vinginevyo, mambo yakiharibika inaweza ikawa vigumu kutowajibika kwa namna moja au ingine.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI


 



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.