• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Wananchi wa kikombo waipongeza Serikali kwa kuanzisha kliniki tembezi

Imewekwa tar.: August 16th, 2019

Wananchi wa Kijiji cha Kikombo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha huduma ya kiliniki tembezi ambayo inatoa huduma za afya karibu na maeneo wanayoishi jamii.

Hayo yamesemwa na Diwani wa Kata ya Kikombo Mhe. Yona Kusaja wakati wa uzinduzi wa kiliniki tembezi uliyofanyika leo katika Kituo cha afya Kikombo kilichopo katika Kijiji cha Kikombo, Kata ya Kikombo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Mhe. Kusaja amesema kuwa ujio wa kiliniki tembezi umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa wataalam waliobobea katika magonjwa mbalimbali hivyo kuwafanya wananchi  wengi  kujitokeza  kwa ajili ya kufanyiwa vipimo  na kupatiwa  tiba kwa haraka na wakati kwa gharama nafuu.

“Wazee wengi wamejitokeza kuja kuchunguzwa afya zao jambo ambalo linatia moyo, kutokana na huduma hizo kusogezwa karibu na wananchi na wanatumia gharama ndogo kutibiwa” Amesisitiza Mhe. Kusaja.

Akizindua Kiliniki hiyo Tembezi Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi amewaomba wananchi kutokuwakatisha tamaa watoa huduma za afya nchini bali wawatie moyo kwa kuwa wanafanyakazi ngumu ya kuokoa jamii hivyo hawana budi kuwaombea na kuwajali watumishi hao.

“Watumishi wa kada ya Afya wanafanyakazi katika mazingira magumu ya kuwahudumia wagonjwa na kuficha siri zao, hivyo ifike wakati wananchi watambue kuwa kazi hiyo ni ya kujitolea hivyo tuwatie moyo na kuwaombea kwa mwenyezi mungu” Amesisitiza Mhe. Katambi

Mhe. Katambi amewataka watumishi wa afya kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wa kuwajali na kuwahudumia wananchi kwa upendo ili waweze kuvutiwa na huduma zinazotolewa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Amesema kuwa ni wajibu wa watoa huduma za afya nchini kuhakikisha wanatoa huduma bora za afya  na zenye viwango kwa jamii ili kupunguza malalamiko katika Sekta ya Afya nchini.

Wakati huohuo  Afisa Ustawi wa Jamii Bi. Shekilaga Nkinda kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ambaye pia ni Mlezi wa Timu za Afya Mkoa wa Dodoma) amewaomba wananchi kuhakikisha wanakitumia kituo cha afya cha Kikombo kwa kuwa ni mali yao na kimejengwa kwa ajili ya kuwapatia huduma bora za afya.

Amesema kuwa inasikitisha kuona kuwa kituo kimejengwa kwa gharama kubwa na Serikali lakini bado wananchi wanaenda kupata huduma hizo katika kituo cha afya cha Chamwino na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma jambo ambalo halileti picha nzuri kwa jamii.

“Serikali imetumia gharama kubwa kujenga miundombinu ya kituo hichi cha afya lakini inashangaza kwa mwezi mmoja ni wakina mama 30 tu ndio waliokuja kujifungua hapa, ninawaomba wananchi mkitumie kituo chenu “ Anasisitiza Nkinda

Bi. Nkinda amewaomba wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu ya kituo hicho na pia wanatoa taarifa kwa viongozi pale wanapoona huduma zinazotolewa katika kituo hicho zipo nchi ya viwango vinavyohitajika.

Amewaomba wananchi kuhakikisha wanajiunga na bima ya afya ili waweze kupata huduma za afya kwa urahisi pale wanapokuwa hawana fedha.

Hata hivyo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dkt. Gatete Mwihava amesema kuwa wamebuni huduma ya kiliniki tembezi ili iweze kuwasaidia wananchi maskini kwa kuwaletea wataalam wa magonjwa mbalimbali ili kuwapunguzia gharama za kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

Amesema huduma ya kliniki tembezi inawataalam wa macho, meno, wataalam wa afya ya mama na mtoto, magonjwa yasiyoambukizwa, saratani ya kizazi na matiti, na hivyo huduma hiyo itaendelea kutelewa katika Halmashauri zote za Jiji la Dodoma.

Aidha, ikumbukwe kuwa, Ofisi ya Rais TAMISEMI ilishatoa maelekezo kwa Timu za Afya Mikoa na Halmashauri nchi nzima kwamba, wahakikishe wanazingatia kuanzisha huduma za Kliniki Tembezi ili, kuwapunguzia mzigo wananchi kufuata huduma mbali na makazi yao.

Na. Angela Msimbira KIKOMBO



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.