• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano Kuanza Masomo Julai 20, 2020

Imewekwa tar.: June 17th, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema wanafunzi wote wa bweni waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano kwa mwaka 2020 wanatakiwa kuripoti shuleni tarehe 18 Julai,2020 na wale wa kutwa kuripoti na kuanza masomo tarehe 20 Julai,2020.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kuhusu uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ualimu na vyuo vya ufundi mwaka 2020 mapema leo katika Ofisi za TAMISEMI, Jijini Dodoma.

Amesema wanafunzi ambao hawataripoti wiki mbili tangu tarehe ya kufungua shule nafasi zao zitachukuliwa na wanafunzi wengine ambao hawakupangiwa shule katika awamu hii.

Aliongeza kuwa Uhamisho wa shule utaruhusiwa baada ya kukamilika kwa muhula wa kwanza wa masomo, na zoezi hilo litafanyika kwa kuzingatia uwepo wa nafasi kwenye Shule kwa idhini ya Maafisa Elimu wa Mkoa husika, hivyo hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya shule kwa sasa ngazi za Mikoa, Halmashauri na Shule.

Akizungumzia takwimu za watahiniwa wa mtihani wa kidato cha Nne,2019 amesema watahiniwa wa shule 425,072 wakiwemo wasichana 221,813 na wavulana 203,259 walifanya mtihani wa kuhitimu kidato cha Nne mwaka 2019 na watahiniwa wa kujitegemea walikua 48,683.

“Jumla ya wanafunzi 121,251 wakiwemo wasichana 53,829 na wavulana 67,422 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), idadi hii ni sawa na asilimia 93.4 ya wanafunzi wenye sifa za kuchaguliwa alisema Waziri Jafo”

Aidha Waziri Jafo alifafanua kuwa  wanafunzi 73,101 wakiwemo wasichana 35,005 na wavulana 38,096 sawa na asilimia 52.1 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na wanafunzi 9,264 wakiwemo wasichana 4,314 na wavulana 4,950 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Elimu ya ufundi, vyuo vya Afya na vyuo vya Ualimu huku wanafunzi 38,886 wakiwemo wasichana 14,510 na wavulana 24,376 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Elimu ya ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).


Waziri Jafo alitoa maelekezo kwa wanafunzi waliopangwa kwenye vyuo vya Elimu ya Ufundi vilivyopo chini ya NACTE kuwa wanatakiwa kuthibitisha kukubali kujiunga na kozi zinazosimamiwa na NACTE baada ya siku saba kuanzia siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi hadi tarehe 15 Agosti 2020.

“Mwanafunzi atafanya uthibitisho kupitia kiunganishi kinachoitwa UTHIBISHO TAMISEMI katika tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ambayo ni www.nacte.go.tz ili kukubali kuchaguliwa kwenye kozi za vyuo walivyopangiwa.

Mwanafunzi ambaye hatathibitisha kukubali nafasi aliyochaguliwa, nafasi yake itachukuliwa na wanafunzi wengine wanaoendelea kuomba katika vyuo hivyo kwa njia ya mtandao” Alisema Waziri Jafo.

Aliongeza kuwa wanafunzi wanaotaka kufanya mabadiliko ya kozi au chuo walichochaguliwa wanaruhusiwa kufanya hivyo kuanzia tarehe 01 Agosti hadi 30 Agosti 2020 kupitia mtandao wa NACTE.

Aidha Waziri Jafo alibainisha kuwa wanafunzi waliopangwa katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya hawatahusika na utaratibu wa kubadilisha wa NACTE, hivyo wanapaswa kuwasiliana na vyuo husika.

Pia Waziri Jafo aliwashukuru wadau wote wa Elimu kwa kushiriki kikamilifu kuimarisha miundombinu ya shule ikiwemo madarasa, mabweni, maktaba,maabara na majengo mengineyaliyowezesha shule 32 mpya kuanzishwa na kupokea jumla ya wanafunzi 2,571 wakiwemo wasichana 1,584 na wavulana 987 wa kidato cha Tano kwa mara ya kwanza.

Alihitimisha kwakuwataka wakurugenzi wa Halmashauri za Kyerwa Dc, Momba Dc, Mtwara Dc, Ubungo Mc na Nanyamba Tc ambazo hazina shule za kidato cha Tano na Sita kuhakikishe kuwa kufikia tarehe 30 Januari, 2021 Halmashauri zao ziwe na  Shule zenye Kidato cha Tano hususan za masomo ya Sayansi na Hisabati na ziwe zimetengewa bajeti ya chakula.

Mwisho.


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Kafanyeni Tohara kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi

    March 04, 2021
  • Uhaba wa Saruji wachelewesha ujenzi wa barabara za Mji wa Serikali

    March 03, 2021
  • Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

    March 03, 2021
  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.