• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Walimu Wakuu shule za msingi watakiwa kusimamia fedha zinazotolewa na Serikali

Imewekwa tar.: January 5th, 2021


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amewataka walimu wakuu wa shule za msingi nchini kuhakikisha wanasimamia fedha zinazotolewa na Serikali  kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu  kwa kufuata sheria na taratibu katika matumizi.

Akifungua mkutano mkuu wa pili wa umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania Bara leo, Jijini Dodoma Mhandisi Nyamhanga amesema serikali inapeleka fedha  za ruzuku mashuleni kwa kila mwezi ili ziweze kununua vifaa vya kufundishia, kujifunzia hivyo ni jukumu la  walimu  kusimamia kwa umakini na kuhakikisha wanafunzi hao wanapata elimu bora.

Mhandisi Nyamhanga anafafanua kuwa Serikali inafanya kila linalowezekana kuhakikisha elimu ya msingi hapa nchini inakuwa bora kwa kuboresha miundombinu ya elimu, hivyo ni wajibu wa Wakuu wa Shule za Msingi kuhakikisha fedha hizo zinasimamiwa kikamilifu.

“Serikali iko makini kuhakikisha suala la elimu linakuwa mbele zaidi kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maboresho ya miundombinu katika ujenzi wa vyoo,nyumba za walimu na mabweni ni kazi yenu kuhakikisha fedha hizo zinasimamiwa ili ziweze kutumika katika miradi iliyokusudiwa ,”amefafanua Mhandisi Nyamhanga

Mhandisi Nyamhanga amesema Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha elimu ya msingi na kusisitiza kuwa fedha za programu ya elimu bila malipo zitatumika kufidia malipo ya ada,posho kwa walimu wakuu pamoja na huduma nyingine za msingi.

Aidha, Nyamhanga ametumia fursa hiyo kuweka wazi kuwa Serikali inalaani vitendo vya udanganyifu wa mitihani na kuwataka walimu wakuu nchini kuendelea kudhibiti vitendo hivyo ili kuboresha elimu ya msingi.

“ Ni jambo la kusikitisha kuona katika ulimwengu huu bado walimu hamuwezi kudhibidi wizi wa mitihani,tunawakatisha tama wanafunzi wanaojituma,”amesema Mhandisi Nyamhanga.

Mhandisi Nyamhanga amesema vitendo vya udanganyifu wa mitihani bado ni tatizo ambalo lipo linatia doa  doa  kubwa kwani kwa kipindi cha mwaka jana pekee jumla ya wanafunzi 1065 walifutiwa matokeo ya mitihani kwa udanganyifu na kuwataka walimu hao wakuu kuangalia namna ya kudhibiti na kwamba hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa watakaovujisha .

Wakati huo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais –TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Gerald Mweli ametoa rai kwa umoja huo kujituma katika kutoa elimu bora kwa jamii ili kuzalisha wataalamu watakaotosha nchini.

Naye Rehema Ramole Mwenyekiti wa umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania Bara ameishukuru serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kulipa walimu mishahara yao kipindi chote shule zilipofungwa kutokana na ugonjwa wa Corana.


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Vikundi 47 Kondoa vyapewa mikopo ya shilingi milioni 147

    February 24, 2021
  • Mikopo ya Shilingi Milioni 85 yatolewa kwa Vikundi wilayani Bunda

    February 24, 2021
  • Mradi wa Fursa na Vikwazo Iliyoboreshwa Kuingizwa kwenye Majukumu ya OR - TAMISEMI

    February 23, 2021
  • Mikopo ya Sh. Milioni 850 yatolewa kwa Vikundi 104 jijini Tanga

    February 15, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.