• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Uwekezaji kwenye Elimu waanza kuzaa matunda

Imewekwa tar.: July 12th, 2019

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ametoa siri ya shule za serikali kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2019, akidai kuwa ni kutokana na uwekezaji uliofanywa kwenye sekta ya elimu.

Akizungumza na jana na waandishi wa habari ofisini kwake jijini hapa, Jafo alisema shule hizo zimefanya vizuri ikilinganishwa na awali ambapo ufaulu wake haukuwa mzuri.

“Hapo awali ulikuwa ukiangalia shule 100 bora, shule za serikali zilikuwa za kutafuta…Siri kubwa ya mafanikio ya shule za serikali kufanya mapinduzi makubwa ni uwekezaji katika elimu,”alisema.

Alisema serikali imewekeza katika miundombinu ya elimu ambayo kwasasa ni rafiki, uwepo wa vifaa vya maabara na mabilioni mengine ya fedha yameingizwa kwenye ununuzi wa vifaa hivyo.

“Tumewekeza pia katika rasilimali watu, tumeongeza idadi ya walimu leo hii, shule zina walimu 40-30 wakati zamani zilikuwa zina walimu 5-7, kuna shule hadi walimu wengine wanabadilishana vipindi, tulikuwa na changamoto ya walimu wa sayansi ambayo tunaendelea kuwekeza huko na wanafunzi wameanza kufanya vizuri,”alisema.

Waziri Jafo alisema shule za kata hali yake ya awali haiwezi kulingana na sasa ambapo kuna walimu wa kutosha huku akiwataka wazazi kuwaacha watoto kusoma kwenye shule wanazochaguliwa.

“Usione mtoto amepelekwa shule ya kata ukadharau, kumbuka shule hii inaweza kupiga bao leo hii tuangalie shule ya Lukole matokeo yake linganisha na Jangwani au Azania, tusihamishe watoto tuwaache wasome, serikali imeweka uwekezaji mkubwa, niwatoe hofu watanzania tunaenda sasa sehemu nzuri na salama,”alisema.

Alifafanua kuwa ufaulu umeendelea kuimarika ambapo umepanda kutoka asilimia 98.2 hadi 98.93 na kwamba katika shule 10 bora za kwanza shule nne ni za serikali.

“Hii ni faraja kubwa sana kwa mwaka wa pili mfululizo tumeona Kibaha ambayo mwaka jana ilikuwa ya kwanza, shule nyingine Kisimiri ambayo ni shule ya kata kihistoria sasa imekuwa ya kwanza,”alisema.

Waziri huyo alitaja shule hizo nne zilizoingia 10 bora kuwa ni Kisimiri, Mwandeti, Tabora boys na Kibaha.

“Kwa hiyo haya ni mafanikio makubwa ambayo tumedhamiria kuyafanya, tumeona shule hizi mbili zina asili ya kata, niwapongeze walimu na wanafunzi kwa kuweza kufanya vizuri,”alisema.

Aidha alisema nafasi ya 11 hadi 20, shule sita za serikali ambazo ni Ilboru, Nachingwea, Mzumbe, Mwanamwema, Tabora girls na Dareda.

“Shule hizi zinafanya vizuri ikilinganishwa na kule tulikotoka mwanzo, pia katika shule 100 bora mwaka huu shule 64 ni za serikali ambazo 52 ni za kata na 12 ni shule kongwe na vipaji maalum,”alisema.

Alisisitiza kuwa shule za kata kwasasa zinatimua mbio licha ya wengine walikuwa wakizibeza.

“Wazazi acheni watoto wasome kwenye hizo shule serikali imeweka mazingira rafiki kupeleka vifaa na walimu na haya ndo matunda makubwa ya serikali,”alisema.

Kadhalika, alisema katika wanafunzi 10 bora watano wametoka shule za serikali na wanafunzi watano bora wa masomo ya sayansi ni shule za serikali.

Alipongeza mikoa mitatu ambayo ni Arusha, Tabora na Pwani ambazo shule za serikali zimefanya vizuri kwa kuingia 10 bora.

“Nimpongeze Mkuu wa mkoa wa Pwani anajitahidi sana kuna shule pale inaitwa Maneromango ndo imetoa kwa mara ya kwanza wanafunzi wa kidato cha sita imefanya vizuri imekuwa shule ya 59 kitaifa kati ya shule 594, na ni shule ya pili kwa mkoa wa Pwani ukiacha Kibaha,”alisema.

Alisema ataandaa vyeti maalum kwa wakuu wa mikoa hiyo mitatu huku akiagiza tathmini ifanyike kwa mikoa iliyofanya vibaya ili kutafutia ufumbuzi changamoto zinazokwamisha ufaulu.

“Ifanyike tathmini mkoa wa Mara takribani shule 3 zipo kwenye kundi la ambazo hazijafanya vizuri, tujue nini kimejitokeza kwenye shule zile ili yale yote madhaifu tuyafanyie kazi wafanye vizuri zaidi, na ifikapo 2020 kutakuwa na mapinduzi makubwa kwenye elimu,”alisema.

Mwisho.



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

    January 22, 2021
  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.