• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Undikishaji wa Wapigakura Wavunja Rekodi

Imewekwa tar.: October 18th, 2019

UANDIKISHAJI wa orodha ya wapigakura wa uchaguzi wa Serikali za mitaa umevunja rekodi baada ya zaidi ya watu milioni 19.7 ambayo ni sawa ya asilimia 86 ya malengo yaliyowekwa kujitokeza kujiandikisha huku mkoa wa Dar es Salaam ukiwa kinara kwa kuandikisha kwa asilimia 108.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ilikadiria kuandikisha Wapigakura 22,916,412 ambao ni sawa na asilimia 85 ya Wananchi wenye sifa za kupigakura ambao kati hao Wanaume 10,924,479 na Wanawake 11,991,933.

Kutokana na kufanya vizuri kwa Mikoa yote, wakuu wa Mikoa na Wilaya kumemfanya Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo kusitisha maamuzi yake ya kupeleka Dokezo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli la kuchukuliwa hatua za kinidhamu endapo wangeshindwa kuhamasisha na wangeandikisha chini ya asilimia 50.

Akitoa tathimini ya siku 10 za uandikishaji wapigakura, Jafo alisema wapigakura 19,681,259 wameandikisha ambayo ni sawa na asilimia 86 ya lengo la kuandikisha wapigakura 22,916,412.

Jafo alisema hadi kufika Oktoba 17 mwaka huu, wapigakura zaidi ya milioni 19.68 wamejiandikisha wanaume wakiwa ni 9,529,990 na wanawake ni 10,151,267 ambao ni sawa na asilimia 86 ya lengo la kuandikisha wapigakura zaidi ya milioni 22.9.

Uandikishaji wa mwaka huu umekuwa na mafanikio ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2014 ambapo walioandikishwa walikuwa ni 11,882,086 ambayo ilikuwa ni asilimia 63 ya makadirio ya kuandikisha wapigakura 18,787,820.

Waziri Jafo alibainisha changamoto zilizojitokezwa  wakati wa zoezi la uandikishaji  kuwa ni hali ya mvua katika baadhi ya maeneo pamoja na ile ya wananchi kuchanganya na zoezi la uboreshaji wa Dafari la Kudumu la wapiga kura na baadhi ya vituo kuwa mbali na kuwa ngumu kwa wananchi kufikiwa.

Alifafanua kuwa kutokana na changamoto hizo siku za uandikishaji ziliongezwa kutoka kuwa siku saba mpaka kufukia siku kumi hivyo zoezi hilo lilifanyika kuanzia Tarehe 7 – 17/10/2019.

Akizungumzia takwimu za uandikishaji wapigakura kimkoa, Jafo alisema jumla ya mikoa 26 imeshiriki katika zoezi la uandikishaji ambapo Dar es Salaam ilishika nafasi ya kwanza kuandikisha wapigakura 2,892,535 ambayo ni asilimia 108.

Alisema Dar es Salaam imefuatiwa na Mkoa wa Pwani ulioandikisha 568,627 (asilimia 96), Mwanza iliyoandikisha 1,340,177 sawa na asilimia 95, Tanga iliyoandikisha 983,104, Singida iliyoandikisha 610,344 ikiwa ni kwa asilimia 90 kila mmoja na Morogoro iliandikisha 1,075,379 sawa na asilimia 89.

Mikoa mingine ikionyesha na idadi ya wapiga kura ni Mbeya 776,811 (asilimia 83), Ruvuma 651,257 (asilimia 88), Katavi 243,163 kila ni sawa na asilimia 88 kila mmoja.  Mtwara 604,670 (asilimia 86), Dodoma 893,890 (asilimia 85), Rukwa 410.760 (asilimia 85) na Arusha 787,232 (asilimia 85).

Mingine ni Lindi iliyoandikisha 396,832 (asilimia 84), Iringa 433,259 (asilimia 84), Mara 673,065 (asilimia 80), Kilimanjaro 741,130 (asilimia 79), Geita 664,100 (asilimia 79), Manyara 565,827 (asilimia 78), Tabora 876,664 (asilimia 78), Songwe 402,840 (asilimia 78), Kagera 961,520 (asilimia 78), Shinyanga 583, 928 (asilimia 76), Simiyu 568,342 (asilimia 76), Njombe 290,791 (asilimia 75) na Kigoma 676,012 (asilimia 65).

Sambamba na hili, Jafo alitoa cheti na kombe kwa mikoa na halmashauri zilizofanya vizuri katika uandikishaji wa wapigakura wa uchanguzi wa serikali za mitaa.

Jafo alitaja mikoa iliyofanya vizuri na iliyopewa kombe na mingine cheti kuwa ni pamoja na Dar es Salaam iliyoandikisha kwa asilimia 108, Pwani kwa asilimia 96, Mwanza kwa asilimia 95, Tanga kwa asilimia 90, Singida kwa asilimia 90.

Kwa upande wa halmashauri Jafo alizitaja na kuzitunikia halmashauri tano ambazo ni Mlele DC iliyoandikisha wapigakura 27,196 (asilimia 152), Ngorongoro DC iliyoandikisha 96,622(asilimia 129), Kibiti DC iliyoandikisha 60,539 (asilimia 126), Temeke iliyoandikisha 879,619 (asilimia 122) na Monduli iliyoandikisha 91,363(asilimia 122).

Wakati huo huo Jafo alitaja halmashauri 5 zimefanya viziri kuandikisha waandishi wengi zaidi kuwa ni Temeke ambao wameindikisha wapigakura 879,619 (asilimia 122), Ilala iliyoandikisha wapigakura 820,600(asilimia 111) manispaa ya Mwanza iliyoandikisha 224,901(asilimia 105), Ubungo MC imeandikisha 542,728 (asilimia 103) na Kinondoni iliyoandikisha 569872(asilimia 96).

Aidha, Jafo ametumia fursa hiyo kutaka hamasa iliyotumika kushawishi wananchikujiandikisha ndiyo itumike wakati wa kupiga kura.

“Ni imani yangu watu wengi pia watajitokeza wakati wa kupiga kura ya kuwachangua viongozi ambao ndio msingi wa maendeleo ya wananchi,” alisema.

Jafo amewataka watanzania kuendeleza amani na utulivu wakati wa kuchukua fomu, kurudisha fomu na kupiga kura huku akisisitiza kujiepusha na vitendo vya rushwa kwa wagombe na wapigakura.

Aidha Jafo amewaposhukuru viongozi wote waliojitokeza kujiandikisha kwenye Orodha ya Daftari la Wapigakura kuanzia gazi za Taifa, Mikoa,Wilaya, Halmashauri, Tarafa, Kata, Mitaa, Vijiji na vitongoji na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi hatimaye kufanikisha zoezi hili.

Uchaguzi wa serikali za mitaa umepangwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu na utafanyika katika vijiji 12, 319, mitaa 4,264 na vitongoji 64, 384

Na. Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI


Matangazo

  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Tangazo la kazi kada ya Afya January 20, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Mweli awatega Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu kwenye Mfumo wa PREM/PREMS.

    January 10, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.