• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu

Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

Imewekwa tar.: January 20th, 2021

Na Atley Kuni, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani S. Jafo ameuagiza uongozi wa Jiji la Dodoma kufanya ukarabati wa Shule ya Msingi Nkuhungu iliyopo katika Jiji hilo ndani ya siku 14 ili kumaliza adha ya wanafunzi kusoma katika mazingira yasiyo rafiki kwao.

Waziri Jafo amefikia hatua hiyo hii leo tarehe 20 Februari, 2021 alipofanya ziara katika shule hiyo ambapo ilimlazimu kutoa maelekezo ya awali, alipovinjari darasa la awali na kukuta halina paa wala michoro ambayo ingeweza kuwasaidia Watoto kujifunza kwa weledi.

“Hili ni darasa la awali nilitegemea nikiingia humu, nione michoro ya aina mbalimbali ambayo inamsaidia Mwalimu anapofundisha na pia inakuwa rahisi kwa mtoto kujifunza kwa wepesi. Sasa naagiza darasa hili likarabatiwe kwa kupigwa plaster, na rangi lakini pia ichorwe michoro ya vitu mbali mbali” alisema Jafo.

Akiwa anaendelea na ziara yake katika shule hiyo, alilazimika kufanya kikao cha pamoja cha Walimu na Wanafunzi, ambapo alijitolea kuwa mlezi wa shule hiyo na kuutaka uongozi ufanye marekebisho kwenye vyumba 16 vilivyojengwa pamoja na darasa moja lililojengwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Antony Mavunde.

“Lakini agizo langu mimi nataka  mkamilishe ukarabati wa shule hii, nawapa wiki mbili  mimi nitarudi hapa tena tarehe 20 Februari,2021, kwa ajili ya kuona ukarabati uliofanyika, maana hapa mkijipanga vizuri sio zaidi ya shilingi milioni 25 mtabadili kabisa mazingira ya kufundushia na kujifunzia Amesema Jafo.

Awali akisoma taarifa ya shule, Mkuu wa Shule ya Msingi Nkuhungu, Bernard Chanai, amesema kutokana na wingi wa wanafunzi katika shule yao, mpango uliopo sasa ni kujenga shule mpya mbili katika eneo la Ndachi ili kupunguza idadi ya wanafunzi na kufikia lengo la kisera la kuwa na wanafunzi 915 kwa shule.

Chanai amesema, Serikali ya awamu ya tano kupitia Halmashauri ya Jiji la Dodoma, walitoa shilingi milioni 545 ikiwa ni mpango wa ndani wa mwaka wa fedha, 2018/19 na 2020/21, fedha ambazo zinafanikisha ujenzi wa shule za Mnyakongo na Mtupe ambazo kila moja imeanza kwa kujengewa vyumba 10 vya madarasa, Matundu 9 ya vyoo sambamba na ujenzi wa jengo la Utawala, ikiwa ni mkakati wa Jiji kukabiliana na wingi wa wanafunzi.

Wakati huo huo Waziri Jafo ametembelea Shule ya Sekondari ya Itega, ambapo akiwa shuleni hapo alionekana kukerwa na hali ya matokeo mabovu ya kidato cha Nne kwa mwaka uliopita, kufuatia shule hiyo kutopata ufaulu wa daraja la kwanza mbali ya shule husika kuwa eneo la mjini.

“Hapa ni mjini miundombinu yote mnayo, mnashindwa vipi na shule nyingine zipo kijijini kabisa, suala hili halikubaliki, lazima muongeze bidii katika kufundisha” aliuambia uongozi wa Shule hiyo pamoja na Walimu.

Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa mbele ya Waziri Jafo, Ufaulu katika Shule ya Sekondari Itega, unaonesha ufaulu kwa mwaka ulipita, ulianzia daraja la pili ambapo ilikuwa ni wanafunzi 3, daraja la tatu wanafunzi 14, daraja la Nne, wanafunzi 62 na sifuri ilikuwa wanafunzi 25.

Akitoa Salamu za Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Benelith Mahenge, alisema mkoa umeendelea kujidhatiti katika suala la elimu kwa kila Wilaya na masuala mengine ya kiuchumi pamoja na suala la ulinzi na usalama.

Waziri Jafo, alikuwa katika ziara ya siku moja katika Wilaya ya Dodoma na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ujumla ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi kote nchini.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu, wakimsikiliza Waziri Jafo, alipo tembelea shule hiyo na kuzumza nao, hayupo pichani

Mhe. Waziri Jafo akiwa picha ya pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Serikali yalegeza masharti mikopo ya asilimia 10

    February 27, 2021
  • Vikundi 23 Wilayani Busega vimenufaika na mikopo ya asilimia 10

    February 26, 2021
  • Vikundi 366 Wilayani Kilwa vyanufaika na mikopo ya sh bilioni 1.1

    February 26, 2021
  • Waziri Jafo ataka Zimamoto, Skauti wakomeshe majanga ya moto shuleni

    February 26, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.