• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Shule 8 za Serikali zaingia kumi bora matokeo ya Kidato cha Sita

Imewekwa tar.: August 21st, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.  Selemani Jafo amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta ya elimu na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli ndio siri iliyopelekea shule nane za serikali kuingia kwenye kumi bora katika matokeo ya kidato cha sita 2020.

Ameyasema hayo leo ofisini kwake Jijini Dodoma wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu ufaulu wa Shule za sekondari zinazomilikiwa na Serikali katika matokeo ya kidato ya sita.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano Serikali imeendelea kufanya vizuri katika Sekta ya Elimu ambapo kwenye matokeo yaliyotangazwa leo tarehe 21/08/2020  ufaulu umeongezeka kwa wanafunzi wa kidato cha sita kutoka  asilimia 98 kwa mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 99.51 kwa mwaka.

Amesema kuwa katika matokeo hayo shule za Serikali nane zimeweza kuingia katika  shule kumi bora kwa mara ya kwanza zikiwemo shule za kata 3 ambazo ni Kasimiri, Mwandeti na Dareda.

Amezitaja shule za Serikali zilizoshika nafasi kumi bora kuwa ni Mzumbe, Shule ya wasichana Tabora, shule ya wavulana Tabora, Iiliboru na  Kibaha

“Zamani ufaulu wa shule za Serikali ulikuwa mdogo  kiasi kwamba wazazi walikuwa hawapendi kuwapeleka watoto wao kusoma katika shule hizo wanapochaguliwa kujiunga na shule hizo, lakini sasa shule hizo zimekuwa na ufaulu mkubwa na kuwa tegemeo  kwa wazazi kuwapeleka watoto wao” amesema Waziri Jafo

Waziri Jafo anafafanua kuwa  uwekezaji uliofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli umeleta mabadiliko makubwa katika eneo la taaluma nchini

Aidha. Jafo amewashukuru waalimu, maafisa elimu Mikoa na Wilaya kwa usimamizi uliotukuka wa kuhakikisha  vijana wa kidato cha sita wanafaulu  vizuri na kuliongezea taifa sifa katika suala zima la sekta ya Elimu.

Amewapongeza Wanafunzi wote wa kidato cha Sita kwa kusoma kwa bidi na kupata ufaulu mzuri japokuwa kulikuwa na  changamoto ya ugonjwa wa CORONA nchi ya Tanzania bado waliweka juhudu katika masomo na kufaulu mitihani yao vizuri.

Waziri Jafo anaendelea kusema kuwa Serikali imetumia kiasi cha shilingi trilioni 1.09 katika suala zima la utoaji wa elimu bila malipo ambayo imehamasisha  sekta ya Elimu nchini,pia kiasi cha shilingi milioni 588 kwa ajili ya  ujenzi wa miundombinu  jambo hili limesaidia kuongeza idadi ya ufaulu wa wanafunzi.

Sambamba na hilo amesema kuwa Serikali imeweza kuongeza idadi ya waalimu  kwa lengo la kuongeza rasilimali ambao  watasaidia kupeleka elimu juu zaidi hali ambayo inapelekea kuongeza ufaulu zaidi nchini.

"Matokeo hayo yameonyesha pia wanafunzi waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ni asilimia 97.74, haya ni mafanikio makubwa,malengo yetu yalikuwa kuingiza shule sita za serikali kwenye kumi bora lakini tumeingiza shule nane,huu ni ufaulu uliozidi viwango" amesema Waziri Jafo.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Viongozi TBA Kigoma matatani kwa kushindwa kukamilisha miradi

    January 18, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.