• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Serikali Yatenga Bilioni 29.9 Kumalizia Maboma Yote ya Shule – Mhandisi Nyamhanga

Imewekwa tar.: February 18th, 2019

Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 29.9 kwa ajili ya kumalizia maboma yapatayo 2,392 nchini kote ili kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka huu wanaanza masomo mara moja kabla ya kumalizika mwezi machi, 2019.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga katika Manispaa ya Musoma leo wakati akiongea na watumishi wa ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Kamati tendaji za Halmashauri ya Manispaa Musoma na Halmashauri ya wilaya Musoma baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika halmashauri hizo hii leo.

“katika kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza na hawakupata nafasi hapa nchini mwaka 2019, Serikali ya Daktari John Pombe Joseph Magufuli imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 29.9 ili kujenga maboma 2,392 ambapo wataweza kuendelea na masomo yao” alisema Nyamhanga.

Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa wanafunzi wapatao 133,737 hawakupata nafasi kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu wa 2019 na ndio Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameamua kutolewa kwa fedha hizo kumaliza tatizo hilo.

Nyamhanga amesisitiza watendaji wote wa mikoa kusimamia fedha hizo na kwamba tayari zimeingizwa katika akaunti za shule husika zenye maboma na hivyo ukamilishaji wa maboma hayo ni lazima uwe wa muda mfupi ili wanafunzi waanze kuanza masomo yao mapema iwezekanavyo. Amesema maboma hayo lazima yakamilike kabla ya kumalizika mwezi machi, 2019 kama ilivyopangwa.

“Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa shule, Bodi za shule na kamati lazima zisimamie fedha hizo, mimi na ofisi yangu tutapita shule hadi shule na kuhakikisha kama fedha zilizopelekwa zimetuka kwa malengo yaliyokusudiwa” alisema Nyamhanga.

Mhandisi Nyamhanga amefanya ziara katika halmashauri ya Manispaa Musoma na Halmashauri ya wilaya Musoma ambapo alitembelea kuona ukarabati mkubwa katika shule za sekondari Songe (wasichana) na shule ya sekondari ya Ufundi wavulana Musoma, miradi ya barabara za TARURA na kituo cha afya Makoko.


                                   Anaandika Fred Kibano


Matangazo

  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Viongozi TBA Kigoma matatani kwa kushindwa kukamilisha miradi

    January 18, 2021
  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.